Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 09Article 541906

Habari za michezo of Wednesday, 9 June 2021

Chanzo: ippmedia.com

Tarimba atingisha kugombea Urais TFF

Tarimba atingisha kugombea Urais TFF Tarimba atingisha kugombea Urais TFF

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Wakili Kiomoni Kibamba, uchaguzi huo utafanyika jijini Tanga Agosti 7, mwaka huu na nafasi zinazogombewa ni Rais wa TFF na wajumbe sita wa Kamati ya Utendaji, ambapo dirisha la kuchukua fomu lilifunguliwa rasmi jana huku likitarajiwa kufungwa Juni 12, mwaka huu.

Rais wa TFF anayemaliza muda wake, Wallace Karia, alishatangaza dhamira yake ya kutetea nafasi yake katika uchaguzi huo ujao, na huenda sasa akakutana na ushindani mkali kutoka kwa Tarimba.

Akizungumza jana baada ya tetesi za yeye kutia nia ya kugombea nafasi ya urais kuzagaa, Tarimba hakukubali wala kukataa, huku akieleza siku bado zipo za kutafakari uamuzi huo.

"Hizo taarifa zipo, watu wengi sana walikuwa wananiomba ama wananishauri, sijui kati ya haya mambo mawili, lakini watu wanalizungumza hilo suala. Siwezi kusema ndiyo ama hapana, lakini kama Mtanzania na kama wenzangu wananiona na mimi najiona kama nafaa, ila hadi sasa sijafanya uamuzi.

"Siku tano bado ni nyingi kama kutakuwa na uamuzi wa kuingia, tutaingia ama kama uamuzi utakuwa siyo kuingia basi hatutaingia, bado ninaendelea kupima," alisema Tarimba.

Kuhusu kuwa njiapanda kutokana na kushindwa kuweka msimamo wake wa kujitosa kugombea ama la, Tarimba alisema: "Hapana sipo njiapanda kwa kuwa suala ni uamuzi na muda, kwa sababu hili jambo limechipuka lazima tulifanyie uamuzi stahiki tuwezi kuona ni jinsi gani tunaweza kuifanyia familia ya soka hapa Tanzania."

Tarimba mbali ya kuwa Mbunge wa Kinondoni, pia ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Kampuni Michezo ya Kubashiri ya SportPesa Tanzania na amekuwa na mchango mkubwa katika soka la nchi hii.

Kwa kupitia SportPesa, kampuni hiyo ni wadhamini wa Klabu za Simba, Yanga na Namungo, lakini pia waliwezesha kufanyika ukarabati mkubwa wa Uwanja wa Benjamin Mkapa ikiwa ni pamoja na kuileta Klabu ya Sevilla ya Hispania kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya 'Wekundu wa Msimbazi' hao.

Join our Newsletter