Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 10 08Article 561955

Soccer News of Friday, 8 October 2021

Chanzo: BBC Sports

Tetesi za Soka 08.10.2021: Bruce, Asensio, Sterling, Dembele, McKennie, Winks, Icardi

Mshambuliaji wa England na Manchester City, Raheem Sterling Mshambuliaji wa England na Manchester City, Raheem Sterling

Manchester City wana nia ya kufungua mazungumzo ya mkataba na Raheem Sterling, 26, na hawataki kumuuza fowadi huyo wa England, ambaye amebakiza chini ya miaka miwili kwenye mkataba wake. (Sun)

Barcelona imekuwa ikihusishwa sana na Sterling na City inamtaka winga wa Ufaransa Ousmane Dembele, 24, kama mbadala wake ikiwa mchezaji wao angehamia Camp Nou. (El Nacional - in Spanish)

Liverpool inafuatilia kwa karibu uhamisho wa winga wa Real Madrid na Uhispania Marco Asensio, 25, ambaye anaripotiwa hana furaha huko Bernabeu. (Mirror)

Wamiliki wapya wa Newcastle wanalenga kuifanya klabu hiyo iwe kubwa kama Manchester City na Paris St-Germain, ambao pia wana wamiliki kutoka Mashariki ya Kati. (Times - subscription required)

Kocha wa zamani wa Chelsea, Frank Lampard na meneja wa Rangers, Steven Gerrard wanazungumzwa kuchukua nafasi ya bosi wa Newcastle Steve Bruce, ambaye anasema anatarajia kupoteza kazi yake. (Telegraph - subscription required)

Juventus wameweka bei ya pauni milioni 25.4 kwa kiungo wa kati wa Marekani Weston McKennie, 23, ambaye anatakiwa na Tottenham. (Calcio Mercato - in Italian)

Mshambuliaji wa Liverpool Divock Origi ameripotiwa kukabidhiwa kwa Barcelona mwezi Januari. Mkataba wa mshambuliaji huyo wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 26 unaisha mwishoni mwa msimu na amekuwa na muda mdogo wa mchezo chini ya Jurgen Klopp. (The Sun)

Kiungo wa kati Harry Winks, 25, anaweza kuhamia Everton kutoka Tottenham mnamo Januari ili kupata wakati zaidi wa kucheza.(CaughtOffside)

Juventus na Inter wanataka kumsajili beki wa pembeni wa Leicester mwenye umri wa miaka 25, Timothy Castagne. (Le Derniere Heure - in French)

AC Milan inataka kumsajili beki wa Ufaransa Samuel Umtiti, 27, kutoka Barcelona mnamo Januari. (Calcio Mercato - in Italian)

Mshambuliaji wa Torino na Italia Andrea Belotti, 27, anaweza kuondoka kilabu humo bure wakati mkataba wake unamalizika(Fabrizio Romano)

Mshambuliaji wa Serbia Dusan Vlahovic, 21, wa Fiorentina, na mshambuliaji wa Paris St-Germain wa miaka 28 Mauro Icardi, 28, wako kwenye rada ya Juventus. (Gazzetta dello Sport - in Italian)

Manchester United na Chelsea wanamlenga mchezaji wa Stoke City Emre Tezgel, 16. Manchester City pia inasemekana inamtaka kijana huyo. (Star)