Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 11Article 584860

Soccer News of Tuesday, 11 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Tetesi za Soka Barani Ulaya, Januari 11

Mlinzi wa Chelsea, Antonio Rudiger Mlinzi wa Chelsea, Antonio Rudiger

Mlinzi wa Chelsea Mjerumani Antonio Rudiger, 28, ambaye mkataba wake unamalizika msimu wa joto na bado hajasaini mkataba mpya na mabingwa hao wa Ulaya, anasemekana kupendelea kuhamia Real Madrid kuliko Paris St-Germain ikiwa ataondoka Stamford Bridge. (Football London)

Rudiger amepokea mapendekezo ya mshahara kutoka kwa Real na PSG, huku klabu hiyo ya Ufaransa ikisemekana kutoa kitita cha Euro milioni 7 kwa mwaka, ambacho ni kikubwa zaidi ya kile ambacho timu ya Uhispania imewasilisha. (Footmercato - in French)

Mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani, 34, ameahidi kujitolea kwa Manchester United kwa muda wote uliosalia wa msimu huu baada ya mazungumzo na mkufunzi Ralf Rangnick. (Mirror)

AC Milan wanafikiria kumnunua beki Mholanzi wa Manchester City, Nathan Ake, 26, baada ya Rossoneri kumpoteza beki wa kati wa Denmark Simon Kjaer, 32, kwa muda wote uliosalia wa msimu huu kutokana na jeraha la goti. (Sun)

Manchester City wanaweza kumfuatilia nahodha wa Croatia Luka Modric, ambaye hajafurahishwa na kuongezwa kwa mkataba unaotolewa na Real Madrid. Mkataba wa sasa wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 katika klabu hiyo ya Uhispania unamalizika mwishoni mwa msimu huu(El Nacional, via Mail)

Arsenal wako tayari kutumia pesa nyingi kumsajili mshambuliaji wa Serbia Dusan Vlahovic, 21 kutoka Fiorentina mwezi Januari. (Mirror)

Paris St-Germain, AC Milan, Roma, Lyon, Barcelona na Newcastle United ni miongoni mwa vilabu ambavyo vinaweza kumtaka kiungo wa kati wa Ufaransa Tanguy Ndombele, 25, ambaye mustakabali wake Tottenham haujulikani baada ya kuzomewa na mashabiki wa Spurs wakati alipolishwa benchi wakati wa Ushindi wa Jumapili wa Kombe la FA raundi ya tatu dhidi ya Morecambe. (Star)

Newcastle United inaweza kushindana na Ajax katika kumsaka winga wa Uholanzi Steven Bergwijn, 24, ambaye wawakilishi wake wanamtazamia kwa mkopo kutoka Tottenham. (90min)

Ajax tayari wametoa ofa ya pauni milioni 15 kwa Bergwijn na wanataka kukamilisha dili kabla ya kumenyana na Utrecht siku ya Jumapili. (Telegraaf - in Dutch)

Newcastle wapo kwenye mazungumzo ya juu zaidi ya kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Hugo Ekitike mwenye umri wa miaka 19 kutoka Reims kwa kima cha chini ya £30m. (90min)

Matumaini ya Newcastle ya kumsajili mlinzi Sven Botman mwenye umri wa miaka 21 wakati wa dirisha la usajili la Januari yanaonekana kukamilika, huku klabu ya Mholanzi huyo ya Lille ikikataa kuwaza kuhusu kuondoka kwake. Mchezaji wa Sevilla wa Brazil Diego Carlos, 28, na Mfaransa Benoit Badiashile, 20, wa Monaco wanasalia kuwa chaguo la Magpies mwezi huu. (Athletic, subscription required)

Tottenham itazingatia ofa kwa kiungo wa kati wa Uingereza Dele Alli, 25, na mlinzi wa Jamhuri ya Ireland Matt Doherty, 29, kuondoka katika klabu hiyo wakati wa Januari. (Sky Sports)

Manchester United wamejadili kumnunua kiungo wa kati wa Borussia Monchengladbach na Uswizi Denis Zakaria mwenye umri wa miaka 25 mwezi huu, lakini dau bado halijatolewa. (Fabrizio Romano)

West Ham wanafikiria kumnunua kwa mkopo beki wa Paris St-Germain raia wa Senegal Abdou Diallo, 25. (RMC Sport - in French)

Mshambuliaji wa Queens Park Rangers, Lyndon Dykes amevutia vilabu kadhaa vya Ligi Kuu ya Uingereza, vikiwemo Newcastle, Burnley, Crystal Palace na Norwich City. Mabingwa wa Scotland Rangers na viongozi wa Ubingwa wa Uingereza Bournemouth pia wanasemekana kumtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Scotland mwenye umri wa miaka 26. (Teamtalk)

Vivianne Miedma, 25, hajakataa kurefusha muda wake wa kukaa na viongozi wa Super League ya Wanawake Arsenal lakini mshambuliaji huyo wa Uholanzi anasakwa na Paris St-Germain na mabingwa wa Ulaya Barcelona. (Telegraph, subscription required)