Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 12Article 585097

Soccer News of Wednesday, 12 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Tetesi za Soka Barani Ulaya, Januari 12

Erling Braut Haaland Erling Braut Haaland

Borussia Dortmund wanatazamiwa kukutana na mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland wiki ijayo huku wakijaribu kujua mipango ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 kuhusu mustakabali wake. (Marca)

Sevilla wamesitisha nia yao ya kumnunua mshambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial kwa vile hawawezi kumudu matakwa ya Manchester United ya kumsajili kwa mkopo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26. (Marca)

Kiungo wa kati wa Paris St-Germain Georginio Wijnaldum amekuwa akihusishwa na Newcastle United lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 31 hana nia ya kurejea katika klabu yake ya zamani. (Football Insider)

Mkufunzi wa zamani wa Tottenham, Jose Mourinho amewasiliana na kiungo wa kati wa Spurs Tanguy Ndombele katika juhudi za kumshawishi kiungo huyo wa kati wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 25 ajiunge naye katika klabu ya Roma, huku klabu hiyo ya Italia ikitaka mkataba wa mkopo na chaguo la kumnunua. (Telefoot, via Mail)

Mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford, 24, anatarajiwa kufanya mazungumzo na Manchester United kuhusu kandarasi mpya, huku mazungumzo yakitarajiwa kuanza kabla ya mwisho wa msimu huu. (Mail)

Crystal Palace wako kwenye mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa Uingereza Eddie Nketiah kutoka Arsenal, huku kandarasi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 ikimalizika msimu wa joto. (Times - subscription required)

Mshambuliaji wa kimataifa wa vijana wa Arsenal na timu ya taifa ya Uingereza Folarin Balogun, 20, anatazamiwa kujiunga na Middlesbrough kwa mkopo kwa muda wote uliosalia wa msimu huu. (Sky Sports)

Brighton na Newcastle United wanapanga kujaribu kumsajili beki wa Argentina Marcos Senesi, 24, kutoka klabu ya Uholanzi ya Feyenoord. (Football Insider)

Brentford na Brighton wamewasilisha ombi la kumnunua mshambuliaji wa Reims mwenye umri wa miaka 19 Hugo Ekitike lakini Newcastle United wanasalia kuwa wanapewa nafasi kubwa ya kumsajili Mfaransa huyo. (90 Min)

Bournemouth inapanga kuwaweka bei wawaniaji wowote wanaoweza kuwania saini ya beki wa Uingereza Lloyd Kelly, huku Everton na West Ham zikimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23. (Football League World)

Tottenham wanataka kusajili beki wa kulia, kiungo na mshambuliaji wakati wa dirisha dogo la usajili la Januari baada ya mkutano kati ya meneja Antonio Conte, mwenyekiti Daniel Levy na mkurugenzi mkuu wa soka Fabio Paratici. (Telegraph - subscription required)

Winga wa Ufaransa Kingsley Coman, 25, anakaribia kusaini mkataba wa kuongezwa na mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich. (Goal)

Chelsea wanafikiria kumrejesha nyumbani beki wa kulia wa Uingereza Dujon Sterling, 22, kutoka kwa mkopo wa msimu mzima huko Blackpool lakini wana hadi Januari 14 kufanya hivyo. (Football League World)