Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 15Article 586123

Soccer News of Saturday, 15 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Tetesi za Soka Barani Ulaya, Januari 15

Nyota wa Klabu ya PSG, Kylian Mbappe Nyota wa Klabu ya PSG, Kylian Mbappe

Tetesi zinasema, Kylian Mbappe, 23, anajadiliana na Paris St-Germain kuhusu mkataba mpya. Mshambuliaji huyo wa Ufaransa wa miaka 23, alitarajiwa kujiunga na Real Madrid kwa uhamisho wa bure wakati mkataba wake utakapokamilika mwisho wa msimu huu.

Erling Braut Haaland anasema kuwa Borussia Dortmund inamshinikiza kufanya uamuzi kuhusu hatma yake. Klabu kadhaa za Ulaya zimehusishwa na uhamisho wa mshambuliaji huyo wa Norway wa miaka.

Tetesi zinasema, Fiorentina wanakaribia kukubali dau la £58m la Arsenal la kumnunua mshambuliaji wa matata wa Serbia Dusan Vlahovic,21.

Tetesi zinasema, Bayern Munich na Barcelona wanataka kumsajili beki wa Chelsea na Denmark Andreas Christensen, 25, wakati mkataba wake utakapokamilika mwishio wa msimu huu.

Tetesi zinasema, Kiungo wa kati wa Tottenham na Ufaransa Tanguy Ndombele,25, anafanya mazoezi mwenyewe na hatma yake ya baadaye katika klabu ya Spurs iko mashakani.

Manchester United wamewasiliana na mkufunzi wa Inter Milan Simone Inzaghi kuhusu uwezekano wa kujiunga nao msimu huu wa joto, huku Muitaliano akikaribia kuanza masomo ya kina ya lugha ya Kiingereza.

Tetesi zinasema, Southampton wameulizia kuhusu usajili mlinda mlango wa Manchester United mwenye umri wa miaka 24 Muingereza Dean Henderson mwezi huu.

Arsenal wamepiga hatua katika mazungumzo yao na Juventus kuhusu usajili wa mkopo wa miezi sita wa kiungo wa kati wa miaka 25-Mbrazil Arthur Melo.

Newcastle United na Watford wanavutiwa na winga wa Nantes Mfaransa mwenye umri wa miaka 24 Ludovic Blas.

Tottenham imewapa Wolves wachezaji wanne kama sehemu mpango wa kumpata winga wa Uhispania Adama Traore, 25.