Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 09Article 584425

Soccer News of Sunday, 9 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Tetesi za Soka Barani Ulaya, Januari 9

Erling Braut Haaland Erling Braut Haaland

Klabu ya Borussia Dortmund inaamini kuwa mchezaji raia wa Norway Erling Braut Haaland, Manchester City itamsajili mchezaji huyo kwenye kipindi cha kiangazi dirisha dogo litakapofunguliwa (Mario Cortegana via Express)

Kiungo wa kati wa Manchester United mreno Bruno Fernandes, 27, huenda akawa mmoja ya wachezaji watakaotua Barcelona ikiwa tu timu hiyo itashindwa kupata kandarasi ya Haaland kwenye kipindi cha kiangazi. (El Nacional, via Mail)

Straika Mhispania Alvaro Morata huenda akasitisha uwepo wa mkopo ndani ya klabu ya Juventus na kujiunga na Barcelona, Ila kocha Massimiliano Allegri ameonesha kutokuwa tayari kumuachia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29, mpaka pale atakapopata mtu wa kurithi nafasi yake. (AS - in Spanish)

Klabu ya Lazio imeonesha nia yake ya kumchukua kipa wa Chelsea Kepa Arrizabalaga lakini mshahara ya Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 27 wa pauni 170,000 kwa wiki ndio unaonekana kuwa kikwazo. (The Athletic - subscription required)

Beki wa Marseille Boubacar Kamara anataka mkataba wa pauni 150,000 kwa wiki kutoka kwa klabu yake msimu ujao,hii ni baada ya West Ham kujiunga na Newcastle katika mnyukano wa kupata saini ya Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 22.(Sun).

Atletico Madrid imeonesha utayari wake wa kumchukua kwa mkopo beki wa kulia wa Arsenal Cedric Soares kwa nia ya kumpatia mkataba wa kudumu Mreno huyo mwenye umri wa miaka 30 majira ya joto. (Mail)

Barcelona imeanza kumwinda winga wa Wolves Adama Traore, 25, ikiwa Mfaransa Ousmane Dembele, 24, ataamua kutoongeza kandarasi yake na timu hiyo ya La Liga, na hivyo kutoa ushindani kwa Tottenham katika majaribio yao ya kumsajili Mhispania huyo. (Diario Sport - in Spanish)

Mshambuliaji wa Fiorentina na Serbia anayekadiriwa kuwa na kiwango cha juu Dusan Vlahovic, 21, yuko tayari kusubiri hadi msimu wa majira ya joto, kuanza mipango ya kuhama na sio kuharakisha kuhama Januari. (90 min)

Beki wa Manchester United na Ivory Coast Eric Bailly, 27, anaweza kulengwa na AC Milan huku wakitafuta mbadala wa beki wa kati wa Denmark Simon Kjaer, 32, ambaye ni majeruhi. (Sky Sports Italy, via Milan Live - in Italian)

Birmingham City wameanza mipango ya kumnunua mshambuliaji wa Manchester United raia wa Ivory Coast Amad Diallo, 19, (Mirror)

Aston Villa, Crystal Palace, Newcastle na West Ham zimeonesha nia ya kusaini kandarasi mpya ya Msenegali ,21, Bamba Dieng wa Marseille. (La Provence, via Sport Witness)

Villa wanavutiwa na kiungo wa kati wa Brighton na Mali Yves Bissouma, ila kocha Graham Potter anasema Seagulls hawatomuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (Birmingham Mail)

Makamu wa rais wa Barcelona Rafa Yuste anasema wachezaji zaidi wanahitajika kuuzwa kabla ya mshambuliaji wa Uhispania Ferran Torres, 21, kusajiliwa Camp Nou baada ya kuhama kutokeaManchester City. (Barca Blaugranes)