Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 19Article 572638

Soccer News of Friday, 19 November 2021

Chanzo: BBC Sports

Tetesi za Soka Barani Ulaya, Novemba 19

Ousmane Dembele Ousmane Dembele

Real wanapanga kushindana na Chelsea, Manchester City na Paris St-Germain kwa kumuongeza mshambuliaji wa Haaland na mshambuliaji wa PSG Mfaransa Kylian Mbappe, 22, kwenye safu ya ushambuliaji ambayo tayari inamshirikisha Mbrazil Vinicius Junior, 21. (AS - in Spanish)

Newcastle United wanapanga kumsajili mlinzi wa Uholanzi Stefan de Vrij, 29, na kiungo wa kati wa Croatia Marcelo Brozovic, 28, kutoka Inter Milan mwezi Januari, pamoja na kipa wa Lazio wa Albania Thomas Strakosha, 26. (Times)

Wakala wa Paul Pogba amedokeza kuwa kiungo huyo wa kati wa Ufaransa, 28, ataondoka Manchester United mwezi Januari, kabla ya mkataba wake kumalizika msimu wa joto. (Rai, via Goal)

Manchester United wanatazamiwa kushindana na Barcelona katika kutaka kumsajili winga wa RB Leipzig wa Kihispania Dani Olmo, 23. (El Nacional - in Catalan)

Chelsea wanavutiwa na mlinzi wa Leicester City Wesley Fofana na wako mbele kidogo ya Manchester United katika kujaribu kumsajili beki huyo wa kati wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 20. (Foot Mercato - in French)

Barcelona wanapanga kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Hakim Ziyech lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka Borussia Dortmund kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Morocco, 28. (Sport,via Metro)

Villarreal wanapanga kukataa ofa zote kwa winga wa Uholanzi Arnaut Danjuma mwezi Januari, huku Liverpool wakimfuatilia mshambuliaji huyo wa zamani wa Bournemouth, 24. (Football Insider)

Manchester United wameanza mipango ya mrithi wao kuchukua nafasi ya kocha Ole Gunnar Solskjaer, huku Brendan Rodgers wa Leicester City akiwa mgombea wanayempendelea zaidi.(Manchester Evening News)

Kocha wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane amejibu maombi ya Manchester United kwa kusema atapatikana mwishoni mwa msimu huu. (Bild, via Express)

Kocha mpya wa Barcelona Xavi anataka kumbakisha mshambuliaji wa Ufaransa Ousmane Dembele lakini amemwambia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 kuwa afanye "sasa au la " kujiimarisha katika klabu hiyo kandarasi yake inapoisha msimu ujao wa joto. (AS - in Spanish)

Nahodha wa timu ya taifa ya England chini ya umri wa miaka 18, Sammy Braybrooke atasaini mkataba na Leicester City licha ya Ujerumani kutaka kumnunua kiungo huyo mwenye umri wa miaka 17. (Athletic, via Leicester Mercury)

Rais wa Barca Joan Laporta "hataondoa" uwezekano wa mshambuliaji wa Paris St-Germain Lionel Messi, 34, na kiungo wa kati wa Vissel Kobe Andres Iniesta, 37, kufuatia mchezaji mwenzao wa zamani Dani Alves kurejea katika klabu hiyo. (Marca-in Spanish) Lionel Messi

Mlinda mlango wa Ujerumani Manuel Neuer ameanza mazungumzo kuhusu kuongeza mkataba wake na Bayern Munich na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 anataka mkataba wa hadi angalau mwaka 2025. (Sport1 - in German).

Mshambulizi wa Real Madrid Gareth Bale, 32, atakuwa nje ya uwanja kwa wiki tatu kutokana na jeraha la mguu baada ya kujiunga na Wales wakati wa mapumziko ya kimataifa. (Marca)