Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 10 07Article 561778

Soccer News of Thursday, 7 October 2021

Chanzo: BBC Sports

Tetesi za Soka Ulaya 07.10.2021:Calvert-Lewin, Watkins, Vlahovic, Lang, Haaland, Winks, Umtiti

Dominic Calvert-Lewin Dominic Calvert-Lewin

Arsenal wanawalenga wachezaji wawili wa England, Dominic Calvert-Lewin,24 na Ollie Watkins, 25, lakini inakabiliwa na kibarua kigumu kuwatoa Everton na Aston Villa katika kuwaachia nyota hao. (Sun)

Manchester City, Chelsea na Manchester United wanajiandaa kumuwania mshambuliaji kinda wa Stoke City, Emre Tezgel, 16, ambaye amekuwa akifananishwa na Harry Kane. (Mail)

Vilabu vya ligi ya Primia vitapambana na Bayern Munich kumnasa kiungo wa kati wa Kijerumani Florian Wirtz anayekipiga Bayer Leverkusen. (Fabrizio Romano)

Liverpool wanafikiria uhamisho wa mshambuliaji wa Serbia Dusan Vlahovic, ambaye mazungumzo kuhusu mkataba wa mchezaji huyo,21, yamevunjika Fiorentina. (Mirror)

Arsenal bado wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Club Bruges Noa Lang, 22, na AC Milan pia inavutiwa naye.(Calciomercato, via TEAMtalk)

Borussia Dortmund wameamua kubaki na mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland, 21, hadi mwaka 2023.(Sport Bild - in German)

Kiungo wa kati wa England na Tottenham Harry Winks,25, anataka uhamisho wa mkopo kutoka kwenye klabu hiyo mwezi Januari na yuko radhi kwenda nje ya England. (Times - subscription required)

Mustakabali wa muda mrefu wa nyota wa Ufaransa, Kylian Mbappe bado utategemea Paris St-Germain baada ya mazungumzo kati ya mama wa mchezaji huyo, 22, kukubali na mabingwa wa Ufaransa kuhusu mkataba mpya kwenda vizuri.(RMC via AS)

Barcelona itamfanya beki wa Ufaransa Samuel Umtiti apatikane Januari hii. Mchezaji huyo wa miaka 27 hajacheza hata dakika moja katika ligi ya La Liga msimu huu. (Sport - in Spanish)

Hisa za 9.5m za Manchester United zilizowekwa kwenye Soko la Hisa la New York na familia ya Glazer zilikuwa na thamani ya pauni milioni 15.7 zaidi kwa sababu ya mshambuliaji wa Ureno mwenye umri wa miaka 36 Cristiano Ronaldo kurudi klabuni. (Mail)