Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 23Article 573604

Soccer News of Tuesday, 23 November 2021

Chanzo: BBC Sports

Tetesi za Soka barani Ulaya Novemba 23

Mauricio Pochettino Mauricio Pochettino

Wachezaji wa klabu ya Paris St-Germain wanaamini kwamba Mauricio Pochettino ataondoka kuelekea Manchester United huku raia wa Ufaransa Zinedine Zidane akimrithi katika klabu ya PSG. (Marca, in Spanish)

United italazimika kulipa Euro Milioni 10 (Pauni milioni 8.4) iwapo wanataka kuvunja mkataba wa Pochettino mwenye umri wa miaka 49 kutoka klabu ya PSG.. (Mirror)

Mkufunzi wa klabu ya Sevilla Julen Lopetegui, 55, ameutaja uvumi unaomuhusisha na klabu ya mchester United kuwa mbaya (Mirror)

Mwenyekiti wa klabu ya Manchester United Ed Woodward anafikiria kuchelewa kuondoka kwake katika klabu ya Old Tarfford ili kusaidia kumtafuta mkufunzi atakayemrithi Ole Gunnar Solskjaer. Mwenyekiti huyo mwenye umri wa miaka 50 anatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo mwisho wa mwaka huu.. (Sky Sports)

Aliyekuwa mkufunzi wa Newcastle Steve Bruce anadaiwa kuwa tayari kuchukua uongozi wa muda mfupi katika klabu ya Manchester United . Raia huyo mwenye umri wa miaka 60 aliichezea Manchester United zaidi ya mechi 300 akiwa mchezaji .. (The Athletic - subscription required)

Mshambuliaji wa Liverpool Mo Salah anakaribia kuandikisha kandarasi ya muda mrefu katika klabu hiyo. Mchezaji huyo ataingia mwaka wa mwisho wa kandarasi yake msimu ujao huku klabu hiyo ikijiandaa kukamilisha masharti mapya ya mkataba wake.. (Team Talk)

Arsenal haitajadili kandarasi ya mkataba mpya na mshambuliaji wa Ufaransa Alexandre Lacazette mwenye umri wa miaka 30 hadi mwisho wa msimu , licha ya kujua kwamba huenda wakampoteza mchezaji huyo kwa uhamisho wa bila malipo.. Atletico Madrid, AC Milan, Marseille na Newcastle zote zinamnyatia mchezaji huyo. (Sun)

Bayern Munich inataka kumsaini mchezaji wa Barcelona mwenye umri wa miaka 18 Pedri, licha ya kiungo huyo wa kati wa Uhispania kuwa na kifungu cha Euro bilioni moja katika kandarasi yake kinachomzuia kuondoka. (AS, in Spanish)

West Ham wanafanya bidi kumsaini mshambuliaji wa Sparta Prague na Czech Republic Adam Hlozek, 19. (Football Insider)

Kiungo wa kati wa klabu ya Lille Renato Sanches anasema yuko tayari kuondoka klabu hiyo ili kupata changamoto mpya.. Arsenal na AC Milan ndio klabu zinazomuwania mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 raia wa Ureno , ambaye alikaribia kutia saini kandarasi na Barcelona msimu uliopita. (L'Equipe, in French)

Mshambuliaji wa Fulham Aleksandar Mitrovic anadaiwa kulengwa na klabu chungu nzima katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari , huku kocha wa klabu ya Villareal, Unai Emery akitarajiwa kumsaini mshambuliaji huyo. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 amefunga magoli 21 katika mechi 18 msimu huu . (Mirror)

Barcelona huenda ikafutilia mbali kandarasi ya mchezaji Samuel Umtiti. Beki huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 28 ameshindwa kukubali pato lililopunguzwa kwa mshahara wake wa Pauni laki 208,000 kwa wiki huku klabu hiyo ikikabiliwa na matatizo ya kifedha.. (Sport, in Spanish)

Bayern Munich inatarajiwa kumpatia kandarasi mpya beki wa Ujerumani Niklas Sule , na kuvunja matumaini ya klabu za ligi ya Premia ambazo zilitaraji kumsaini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kwa uhamisho wa bila malipo.. (TZ, in German)