Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 24Article 573832

Soccer News of Wednesday, 24 November 2021

Chanzo: BBC Sports

Tetesi za soka Barani Ulaya, Novemba 24

Mauricio Pochettino, Pendekezo nama moja la kumrithi Ole Gunner Solskjaer Mauricio Pochettino, Pendekezo nama moja la kumrithi Ole Gunner Solskjaer

Manchester United wako tayari kuacha utafutaji wa meneja wa muda wa klabu hiyo iwapo wanaweza kumpata Mauricio Pochettino kutoka Paris St-Germain kwa wakati huu. (Guardian)

Meneja wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane, nae ni miongoni mwa wanaotazamwa na klabu ya Manchester United anataka kuchukua umeneja katika Klabu ya PSG iwapo Pochettino anaondoka kuelekea Old Trafford. (Telegraph - subscription required)

Meneja wa zamani wa United Sir Alex Ferguson, ambaye ni Mkurugenzi wa bodi ya soka ya klabu hiyo, hatakuwa na jukumu lolote katika kumsaka meneja wao mpya. (ESPN)

Liverpool, Leicester na Newcastle wanamfuatilia kwa karibu mshambuliaji wa Guinea Aguibou Camara mwenye umri wa miaka 20, anayecheza katika klabu ya Olympiakos. (Sun)

Borussia Dortmund wana andaa mkataba mpya kwa ajili ya mshambuliaji Erling Braut Haaland, 21, katika azma ya kumshawishi mchezaji huyo wa kimataifa wa Norway kuendelea kubaki katika klabu hiyo. (Sky Deutschland, in German)

Barcelona wanamtafuta mchezaji wa wa kimataifa wa Morocco anayechezea klabu ya Chelsea Hakim Ziyech, 28, na mshambuliaji Mjerumani Timo Werner, 25, kama wachezaji mbadala kwa mshambuliaji wa Manchester City na England Raheem Sterling, 26. (ESPN)

Newcastle wana nia na kiungo wa kati wa Borussia Dortmund Axel Witsel, 32, na mchezaji wa kimataifa wa ubelgiji, ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu-yuko tayari kuhama. (Sport1, in German)

Mshambuliaji Mbelgiji mwenye umri wa miaka 26 Divock Origi, ambaye analengwa na Newcastle, hataruhusiwa kuondoka Liverpool mwezi Januari. (Northern Echo)

The Magpies (Wachawi) hao wanamtaka beki Kieran Trippier, 31, kutoka Atletico Madrid. (Mirror)

Gerrard anataka kusaini mkataba na mchezaji Pau Torres, 24, kutoka Villarreal. (Fichajes - in Spanish)

Lakini Torres, ambaye alikataa uhamisho ambao ungemlipa pauni milioni 50 iwapo angehamia Tottenham msimu huu, anafurahia kubaki katika klabu yake ya nyumbani kwa sasa. (Guardian)

Meneja mpya wa Aston Villa Steven Gerrard ameidhinisha mauzo mchezaji wa kimataifa wa Burkina Faso Bertrand Traore, 26. (Football Insider)

Mkufunzi wa klabu ya Sevilla Julen Lopetegui, 55, ameutaja uvumi unaomuhusisha na klabu ya mchester United kuwa mbaya (Mirror)

Kiungo wa kati wa Liverpool na Uhispania Thiago Alcantara, 30, amepuuzia mbali uvumi unaomuhusisha na kurudi tena katika klabu yake ya kwanza Barcelona. (Liverpool Echo)

Mchezaji wa kati wa Arsenal na Uswiss Granit Xhaka, 29, atakuwa na nia ya kurejea Borussia Monchengladbach wakati mkataba wake utakapomalizika mwaka 2024. (Mit Geredet, via Mail)