Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 18Article 552193

Soccer News of Wednesday, 18 August 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Timu ya Taifa walemavu, yaomba msaada

Timu ya Taifa ya Walemavu ya Mpira wa Miguu Timu ya Taifa ya Walemavu ya Mpira wa Miguu

Timu ya Taifa ya walemavu ya mpira wa miguu Tanzania Tembo Warriors imeendelea na mazoezi kujiweka sawa na michuano ya Afrika kwa watu wenye ulemavu (CANAF) huku wakiwaomba wadau kuwasaidia vifaa ili kutimiza vema majukumu yao.

Kocha wa Tembo Warriors, Salvatory Edward amesema kuwa wachezaji wake wapo tayari kwa mapambano na wana uhakika wa kufanya  vizuri kwenye michuano hiyo itakayofanyika Novemba hapa nchini.

"Toka nichukue timu hii  kwa kocha aliyekuwepo vijana wameonyesha uwezo mkubwa na sisi kama wenyeji wa michuano hii tunawahakikishia tutapambana na sio kushiriki", amesema Salvatory.

Katika hatua nyingine Salvatory amesema licha ya timu kuendelea na mazoezi bado wana uhaba mkubwa  wa vifaa kama vile mipira, koni na magongo na wanawaomba wadau wawaunge mkono kwani ni jambo la kitaifa.

"Tunaendelea na mazoezi ila vifaa vya mazoezi vimekuwa changamoto  sana kwetu na ukiangalia wachezaji wetu wote ni walemavu hivyo ni ombi langu kwa wadau watuunge mkono kutusaidia vifaa vya mazoezi", amesema Salvatory.