Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 21Article 573211

Soccer News of Sunday, 21 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Tuchel azima tetesi za kuuzwa kwa Ziyech

Hakim Ziyech akiwa na Thomas Tuchel Hakim Ziyech akiwa na Thomas Tuchel

Kocha mkuu wa Chelsea Thomas Tuchel amesisitiza kwamba hakuna mjadala wowote kuhusu kuuzwa kwa Hakim Ziyech bosi huyo pia amesema kwamba taarifa zote zinatengenezwa na watu.

Ziyech hajapata uhakika wa kuanza katika kikosi cha kwanza cha Chelsea licha ya kucheza mechi 39 msimu uliopita staa huyo wa Morocco amecheza mechi 10 pekee msimu huu hali iliyoibua mijadala kwamba Chelsea wana mpango wa kumtoa kwa mkopo wakati wa dirisha la Januari.

Barcelona na Borussia Dortmund wamehusishwa na kuhitaji huduma ya mchezaji huyo, lakini Tuchel amesema:

“Ni rahisi sana kuanzisha mazungumzo. ” Nimeongea mara nyingi alikuwa mzuri sana wakati wa mechi za kabla ya msimualicheza baada ya jeraha la bega na yupo katika kujilinda kwa hiyo imefanya awe huru swala ambalo ni muhimu kwake.

“Sasa ameimarika katika michezo iliyopita. Tulikuwa na majeruhi na alichukua nafasi ya kuwa na muda zaidi wa kucheza kama Callum Hudson-Odoi. Alikuwa na maamuzi. Alisaidia, alifunga, ni vizuri.