Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 19Article 552445

Soccer News of Thursday, 19 August 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Tuisila amrejesha Fiston Yanga

Aliekuwa mvhezaji wa Yanga, Fiston Aliekuwa mvhezaji wa Yanga, Fiston

Kuondoka kwa winga mahiri wa Yanga, Tuisila Kisinda ndani ya Wanajangwani kumemuibua aliyekuwa mchezaji wa timu hiyo Fiston Abdulrazag.

Tuisila alijiunga na Yanga Juni mwaka jana ameuzwa kwa timu ya RS Berkane nchini Morocco akiwa na aliyekuwa mchezaji nyota wa Simba Clatous Chama.

Akizungumza na Mwanaspoti, Fiston amesema kuondoka kwa Tuisila ni pigo kwa Yanga kwa kuwa ndio timu ilikuwa inajijenga na huyo alikuwa nyota muhimu sana.

"Sawa tumeondoka Yanga lakini Tuisila uongozi ungejitahidi kumbakiza, alikuwa muhimu sana katika kupeleka mashambulizi, na ikizingatia Yanga sasa hivi inajijenga zaidi kuwa na kombinesheni nzuri,"

"Sawa kwenda timu nyingine sio mbaya kwa kuwa mpira ndio kazi yake, lakini sio wakati huu, kwanza alianza kuijua na kuisoma Ligi ya Tanzania," amesema Fiston ambaye bado yupo nchini licha ya kuachana na Yanga.