Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 05 28Article 540352

xxxxxxxxxxx of Friday, 28 May 2021

Chanzo: ippmedia.com

Tumekosa magoli mengi - Azam FC

Azam FC imetinga hatua ya nusu fainali baada ya kuwafunga Rhino Rangers mabao 3-1, katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga juzi.

Akizungumza na gazeti hili jana, Vivier alisema mechi yao hiyo ilikuwa na ushindani mkubwa hasa katika kipindi cha kwanza ambacho wapinzani wao walikuwa fiti zaidi na wao walishindwa kutumia vizuri nafasi walizotengeneza.

Vivier alisema kipindi cha kwanza washambuliaji wao hawakuwa na utulivu hali ambayo inawafanya kupoteza nafasi nyingi za kufunga lakini kama wangetumia vyema, wangeibuka na ushindi wa mabao mengi.

"Kama nilivyosema tangu mwanzo kuwa mchezo utakuwa mgumu. Na kweli ulikuwa mgumu. Kwa sababu wakati sisi tukipoteza nafasi Rhino walikuwa na uwezo wa kuuchezea mpira na mpaka wakafanikiwa kutufunga. Ilibidi tufanye kazi ya ziada kukomboa goli na kufunga mengine mawili," alisema Vivier.

Alisema kuwa Rhino walipata bahati kwa sababu wao hawawafahamu vizuri, huku Azam yenyewe ikiwa inafahamika uchezaji wao.

Join our Newsletter