Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 13Article 585439

Soccer News of Thursday, 13 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

"Tunakwenda kubadili historia"- Pablo

Kocha wa Simba, Pablo Franco Kocha wa Simba, Pablo Franco

Kocha Mkuu wa Wekundu wa Msimbazi, Pablo Franco, amesema kuwa wanakwenda kubadili historia ya kufanikiwa kutinga Fainali ya Michuano ya Mapinduzi mara nyingi lakini tumeshindwa kuchukua taji.

Simba katika miaka saba iliyopita wamefanikiwa kutinga fainali mara tano lakini imeshinda ubingwa mara moja pekee suala ambalo Pablo amesema leo ni mwisho.

Pablo amefunguka kuwa kuingia fainali ni jambo zuri lakini kutwaa kombe ni vizuri zaidi hivyo tutahakikisha tunapambana hadi mwisho na kufanikiwa kushinda.

“Tangu mara ya kwanza nilivyokuja hapa nilisema malengo yetu ni kutwaa ubingwa, kesho ni fainali na tuko tayari kupambana kuhakikisha tunafikia dhamira hii.

“Wachezaji wote wako kwenye hali nzuri, tunategemea mchezo mzuri kama ulivyokuwa katika mechi dhidi ya Namungo. Tunataka kuibadili historia na kushinda taji,” amesema Pablo.

Kwa upande wake Nahodha Msaidizi Shomari Kapombe, amesema kila mchezaji yuko tayari kwa ajili ya fainali na lengo ni kutwaa taji.

“Tunajua kila tukifika fainali huwa tunapoteza. Katika miaka ya karibuni tumekuwa hatuna bahati na fainali lakini kesho tutabadili kila kitu,” amesema Kapombe.