Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 13Article 585643

African Cup of Nations of Thursday, 13 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Tunisia Waandika Barua CAF Kupinga Matokeo ya Mali

Benchi la Ufundi la Tunisia wakimlalamikia mwamuzi Benchi la Ufundi la Tunisia wakimlalamikia mwamuzi

Shirikisho la Kandanda nchini Tunisia limeandika barua kwenda katika Shirikisho la Kabumbu Afrika Caf kulalamikia juu ya mapungufu ya kiuamuzi ambayo yalitokea kwenye mechi ya kwanza ya Kundi F katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2021 dhidi ya Mali.

Malalamiko ya Tunisia yanakuja kipindi ambacho mwamuzi wa kimataifa wa Zambia Janny Sikazwe, alifanya kosa la kumaliza mpira kabla ya dakika 90 kukamilika pamoja na makosa kadhaa ya ndani ya dakika alizochezesha, kama kadi nyekundu.

Wakati akimaliza mpira mara zote kabla ya muda (dakika ya 85 na 89) Mali ilikuwa inaongoza kwa goli 1-0 bao la mapema walilofunga katika mbilinge mbilinge hizo za Afcon.

“Tutafanya kila linalowezekana kuhakikisha tunatetea haki zetu za timu ya taifa”, alisema Hussein Jenaieh Ofisa katika Shirikisho la Tunisia.

“Sisi siyo watoto. Kwa sababu barua wameshaipokea hatuwezi kuzungumza zaidi”.

Inaelezwa kuwa moja ya sababu ya kilichotokea ni mwamuzi Sikazwe kutokuwa vizuri kiafya ambapo pia imeelezwa baada ya mchezo huo kumalizika alienda Hospitalini kuangalia afya yake, ndiyo sababu wakati mchezo ukitaka kumaliziwa dakika zilizokuwa zimesalia mwamuzi wa akiba ndiye angechezesha.

Hata hivyo, Shirikisho la Kandanda barani Afrika CAF limesema kuwa linasubili kupokea ripoti za mechi hiyo kabla ya kutoa neno lake kuhusu tukio lile.