Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 21Article 573223

Habari za michezo of Sunday, 21 November 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

“Tutawapiga kama wamesimama”- Try Again

“Tutawapiga kama wamesimama”- Try Again “Tutawapiga kama wamesimama”- Try Again

“Disema 11 tutawapiga kama wamesimama mbinu zote tunazijua” maneno ya Mwenyekiti wa Simba Salim Abdallah ‘Try Again’ akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Simba Ukimbi wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam.

Dongo hilo limetupwa upande wa pili wa watani wao Yanga ambao watakuwana nao kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara Uwanja wa Mkapa Disemba 11, 202. Try Again ameomba ushirikiano wadau wa klabu hiyo kutimiza adhma hiyo.

Try Again Simba ina jeuri ya kusema maneno hayo, kwa sababu wana uhakika na uwekezaji mkubwa ambao umefanywa na unaendelea kufanywa katika klabu hiyo.

“Nasema haya sababu tunayo jeuri. Simba imewekeza kwenye mpira, Simba haijawekeza kwenye kejeli, fitna na vijembe, hayo hayana tija kwetu tumeshapita huko,” amesema Try Again.

"Tutaendelea kuisuka timu yetu ili kuendeleza ubora wake. Tuna timu imara. Mimi na Bodi pamoja na menejimenti tunawashukuru sana. Pressure ilikuwa kubwa lakini tulieni, tupo vizuri sana,” ameongeza "Try Again.