Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 13Article 551446

Soccer News of Friday, 13 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Twiga Stars ratiba hadharani

Kikosi cha Twiga Stars kikifanya mazoezi Kikosi cha Twiga Stars kikifanya mazoezi

Timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake (Twiga Stars) imepangwa Kundi B katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Kusini mwa Afrika kwa Wanawake, ijulikanayo kama COSAFA Cup 2021.

Katika michuano hiyo, Twiga Stars imewekwa kundi moja na Botswana, Sudan Kusini na Zimbabwe.

Kundi A kuna wenyeji, Afrika Kusini, Angola, Malawi na Msumbiji na Kundi C zipo Zambia, Namibia, Eswatini na Uganda.