Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 10 09Article 562264

Boxing News of Saturday, 9 October 2021

Chanzo: eatv.tv

Tyson, Wilder kuzichapa leo kuwania Ubingwa WBC

Tyson, Wilder kuzichapa leo kuwania Ubingwa WBC Tyson, Wilder kuzichapa leo kuwania Ubingwa WBC

Bondia Tyson Fury ametamba kumshushuia kichapo bondia Deontay Wilder kwenye mpambano wa masumbwi wa kuwania mkanda wa ubingwa wa Uzito wa Juu ‘WBC Heavy Weight Championship’ kwenye ukumbi wa T-Mobile Las vegas, Marekani saa 12:30 asubuhi ya kesho Oktoba 10, 2021 kwa saa za Afrika Mashariki

Fury ameyasema hayo baada ya kupima uzito kuelekea kwenye pambano hili usiku w akuamkia leo Oktoba9, 2021 nchini Marekani.

“Nitampiga Deontay kwa KO na itakuwa kwa haraka zaidi kuliko pambano lililopita. Kama alishindwa kunipiga mimi nilipokuwa nje ya uwanja kwa miaka mitatu na kupunguza kilo kumi basi hatonipiga kamwe. Hayupo atakaye weza katika kati yao, sio Wilder, Joshua au Usyk”

“Itakuwa ni uhabaribifu na maangamizi makubwa, na kisha nitamwambie apumzike kwa Amani” Alimalizia hivyo Tyson Fury.

Kwa upande wa Deontay Wilder, yeye amesema, "Utulivu ni siri ya ushindi. Najua nisipokuwa na utulivu akili inatingwa na nafanya maamuzi ambayo siyo sahihi. Lakini nikiwa mtulivu nitashinda na kuwa nitakuwa nafanya maamuzi sahihi”

“Nimejijenga upya mwenyewe, Ukombozi upo mikononi mwetu na nina hamu ya kuuonesha ulimwengu nina kitu gani. Nitajitambulisha upya Dunia nikiwa Deontay Wilder” Amesema Wilder.

Rekodi zinaonesha kuwa, Fury tokea anze masumbwi, amepigana mapambano 31, akishinda mara 30 na kutoa sare mara 1 tena ni mwaka 2018 dhidi ya Wilder ilhali hajawahi kupigwa au kupoteza pambao.

Wakati Deonay Wilder amepigana mapambano 42, ameshinda mara 4, sare 1 na kipigo 1 vyote kutoka kwa Tyson Fury ambapo wawili hao tayari wameshacheza mara mbili, Disemba 2018 naFebruari 2020 ambapo Fury aliibuka naushindi.