Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 10 11Article 562495

Soccer News of Monday, 11 October 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Ufaransa bingwa Uefa Nation League

Mabingwa wa Uefa Nation League Mabingwa wa Uefa Nation League

Kikosi cha vijana wa Didier Deschamps wamenyakua ubingwa wa Uefa Nation league baada ya kuichapa Hispania magoli 2-1.

Mchezo huo ambao umepigwa katika dimba la San Siro nchini Italia umeshuhudia kikosi cha Hispania kikionesha soka safi na ndio waliokuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 64, lililowekwa kimiani na Mikel Oyarzabal.

Haikuchukua dakika nyingi Ufaransa wakasawazisha kupitia kwa nyota kutoka klabu ya Real Madrid, Karim Benzema akifunga goli safi dakika ya 64.

Ni Kylian Mbappe ndie aliewahakikishia Ufaransa kunyakua kikombe baada ya kupachika goli la ushindi dakika ya 80, na kufanya mechi hiyo kumalizika 2-1.

Katika mchezo mwingine Italia wamekamata nafasi ya tatu baada ya kuifunga ubelgiji magoli 2-1 .

Magoli ya Italia yamefungwa na Nicolo Barella na D. Berardi kwa mkwaju wa penati, huku lile la Ubelgiji likifungwa na Ketelaere.