Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 28Article 560104

Soccer News of Tuesday, 28 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Ufundi na mipango bao la Mayele

Mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele akiwaacha mabeki wa Simba wakiwa hawaamini Mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele akiwaacha mabeki wa Simba wakiwa hawaamini

Baada ya kufunga bao ambalo liliipa ushindi Yanga dhidi ya Simba katika mchezo wa Ngao ya Jamii, mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele amelichambua bao lake ambalo alimfunga kipa wa Simba, Aishi Manula katika mchezo uliofanyika  Uwanja wa Mkapa Jumamosi, Septemba 25.

Mayele mwenye uraia wa DR Congo amejiunga na Yanga katika dirisha kubwa mwaka huu mpaka sasa amefanikiwa kuifungia Yanga mabao 5 katika michezo 6 aliyoichezea timu hiyo ikiwemo na ile ya kirafiki ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu 2021/22 ulioanza jana Jumatatu.

Mayele amesema kuwa anafuraha kubwa kuweza kuifungia Yanga bao muhimu katika mechi muhimu kwani ilikuwa ndoto yake kuhakikisha anaifunga Simba baada ya kusajiliwa na Yanga huku akilichambua bao lake kwa kusema kuwa ilibidi aunganishe ile pasi ya Farid Musa ili kipa Aishi Manula ashindwe kujipanga kwani kama angetuliza basi anaamini ilikuwa rahisi kwa Manula kuweza kuudaka mpira ule.

“Nafurahi kuona nimefanikiwa kuifunga Simba baada ya kusajiliwa ndani ya Yanga nilitambua moja ya jukumu kubwa kwangu ni kuwapa raha mashabiki wa Yanga kwa kuhakikisha kuwa naifunga Simba, niliahidi nitawafunga na nashukuru Mungu nimefanikiwa katika hilo.

“Kabla sijaupiga ule mpira niliopewa na Musa tayari nilimuona Kipa wa Simba, Aishi Manula akiwa amesogea mbele kupunguza goli hivyo akili ya haraka ilinituma niuunganishe na nisiutulize kwani ningempa kipa nafasi ya kujipanga na mabeki kunizonga hivyo nikaunganisha moja kwa moja nikafanikiwa kufunga nashukuru katika hilo,” amesema Mayele.