Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 10Article 584614

African Cup of Nations of Monday, 10 January 2022

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Ufunguzi wa michuano ya AFCON wafunika

Ufunguzi wa michuano ya AFCON wafunika Ufunguzi wa michuano ya AFCON wafunika

SHAMRASHAMRA za ufunguzi wa mashindano ya 33 ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) katika Uwanja wa Stade Omnisport Paul Biya nchini Cameroon ukiongozwa na Rais wa nchi hiyo, Paul Biya zimefana.

Mwanamuzi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Fall Ipupa na vikundi vya utamaduni vilitumbuiza wakiwa wamevalia mavazi nadhifu ya asili na kuufanya ufunguzi huo kuwa wa aina yake.

Mabingwa wa michuano hiyo mara tano, Cameroon wana matumaini ya kuanza vizuri mbele ya mashabiki wao wakiwa na hamu ya kutwaa ubingwa wa sita.

Akizungumza wakati wa ufunguzi huo jana, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Cameroon, Samuel Eto’o alisema ari ya mashabiki ipo juu hivyo utawala wake utahakikisha kombe linabaki nchini kwao na kuungwa mkono na mashabiki wa soka nchini humo.

“Ni furaha kubwa kwetu Cameroon kuwakaribisha watu kutoka nchi nyingine kwa ajili ya mashindano haya makubwa,” alisema.

Erik Frederick ambaye anacheza kama kipa wa moja ya timu bora katika mji wa Limbe nchini humo amesema anasubiri kupata picha ya nyota Mohamed Salah wa Misri na Sadio Mane wa Senegal kwani amekuwa akiwaona kwenye televisheni.

“Labda naweza kuzungumza nao, kuwasalimu. Nitakuwa na furaha sana,” alisema.

Hii ni mara ya kwanza kwa Cameroon kuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika.

Mara ya mwisho kwa Cameroon kuchukua kombe hilo ni 2017, hivyo wana matumanini ya kulitwaa tena baada ya kufanya hivyo mwaka 1984, 1988, 2000 na 2002.

Katika mchezo wa leo, Senegal itawakosa kipa Edouard Mendy na beki Kalidou Koulibaly kutokana na corona watakapokutana na Zimbabwe.

Mendy, beki wa kati Koulibaly na mshambuliaji Famara Diedhiou wote wako karantini.

Mashindano hayo ambayo yanashirikisha mataifa 24 katika makundi sita yenye timu nne kila moja na jumla ya michezo 52.