Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 30Article 560464

Soccer News of Thursday, 30 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Usajili wa Chirwa umelipa Namungo

Obrey Chirwa Obrey Chirwa

Ni kama Kikosi cha Kutoka Kusini mwa Tanzania Namungo FC hawakufanya makosa Kumsajili aliekuwa mshambuliaji wa Azam FC, Obrey Chirwa.

Ingizo jipya ndani ya Namungo FC, Obrey Chirwa ameweka rekodi yake kwenye mchezo wa kwanza wa ushindani baada ya kutoa pasi mbili za mabao wakati timu hiyo iliposhinda mabao 2-0 dhidi ya Geita Gold.

Chirwa ambaye aliibuka Namungo FC akitokea Azam FC, aliwahi kucheza pia ndani ya Yanga, alitoa pasi ya kwanza kwa mshikaji wake Shiza Kichuya dakika ya 13 na pasi ya pili alitoa kwa Reliants Lusajo ambaye alipachika bao hilo dakika ya 80 na pasi zote Chirwa alitoa kwa mguu wa kulia na alikuwa nje ya 18.

Wakati Chirwa akiandika rekodi yake hiyo nyota wa Mbeya Kwanza, Willy Edgar anashikilia rekodi ya kuwa mfungaji wa kwanza ndani ya ligi na kipa aliyemtungua kwa mara ya kwanza ni kipa namba moja wa Mtibwa Sugar, Aboutwalib Mshery ambaye kwa msimu wa 2020/21 alikusanya jumla ya clean sheet 14.

Pale Mkwakwani ilikuwa ni vurugu mechi baada ya dakika 90, ubao kusoma Coastal Union 1-1 Azam FC ambapo mabao yote yalifungwa na wafungaji kwa mtindo mmoja ilikuwa kwa kutumia kichwa na walikuwa ndani ya 18.

Alianza Daniel Amoah kupachika bao dakika ya 48 lilisawazishwa na Hance Masoud dakika ya 89 na kufanya timu hizo kugawana pointi mojamoja katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.