Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 25Article 553696

Soccer News of Wednesday, 25 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Uwanja wa CCM Kirumba wafanyiwa ukaguzi

Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza

Meneja wa Leseni za Klabu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jonas Kiwia amefanya ukaguzi Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza kama unakidhi vigezo vya kutumika kwa mechi za nyumbani za Biashara United ya Mara kwenye Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Katika ukaguzi huo, Kiwia ameambatana na Mtendaji Mkuu wa Biashara United, Haji Matete, Katibu wa Chama cha Soka Mwanza (MZFA), Leonard Malongo na Katibu wake Msaidizi, Khalid Bitebo.

Biashara United itashiriki Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, na itaanzia ugenini dhidi ya FC Dikhil ya Djibouti kati ya Septemba 10 na 12 kabla ya kurejea nyumbani kwa mechi ya marudiano ya kati ya Septemba 17 na 19 na ikivuka hapo itakutana na mshindi kati ya Hay Alwady Nyala ya Sudan na Al Ahli Tirpoli ya Libya.

Biashara United itautumia uwanja wa CCM Kirumba kama uwanja wao wa nyumbani katika mashindano hayo.