Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 31Article 554632

Habari za michezo of Tuesday, 31 August 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

VIDEO: Breaking: Yanga Yamtangaza Senzo Kuwa Mtendaji Mkuu

Breaking: Yanga Yamtangaza Senzo Kuwa Mtendaji Mkuu play videoBreaking: Yanga Yamtangaza Senzo Kuwa Mtendaji Mkuu

MAKAMU Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Fredrick Mwakalebela leo Agosti 31, 2021 amemtangaza, Senzo Mbatha kuwa Kaimu Mtendaji Mkuu (C.E.O) wa Klabu hiyo atakayesimamia mchakato wa mabadiliko kufikia mwisho na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Yanga, Hajji Mfikirwa atakuwa Mkurugenzi wa Fedha na Utawala.

Mwakalebela amesema Kamati Tendaji wanapenda kumpongeza aliyekuwa Kaimu Katibu wa Klabu hiyo, Hajji Mfikirwa kwa kazi kubwa aliyoifanya ndani ya klabu hiyo.

Akiongea Kaimu C.E.O mpya, Senzo amewashukuru Kamati Tendaji ya Klabu hiyo kwa kumchagua katika nafasi hiyo na atafanya kazi kwa kushirikiana na timu nzima ya Uongozi, wanachama na mashabiki.