Uko hapa: NyumbaniMichezo2019 11 14Article 487795

Sports News of Thursday, 14 November 2019

Chanzo: mwananchi.co.tz

VIDEO-Mgunda: Atetea uamuzi wa kumuacha Manula Taifa Stars

VIDEO-Mgunda: Atetea uamuzi wa kumuacha Manula Taifa Stars

Dar es Salaam. Kocha Msaidizi wa timu ya Taifa Tanzania, Juma Mgunda ametetea uamuzi wa kumuacha kipa wa Simba, Aish Manula akisema kuitwa Taifa Stars ni suala la kila mchezaji mwenye uraia wa Tanzania.

Mgunda aliyasema hayo baada ya kipa wa Simba, Manula kukosekana katika kikosi hiko kwa mfululizo huku akiitwa kipa wa Yanga, Metacha Mnata ambaye hapati namba mbele ya kipa Faroukh Shikhalo.

"Hii ni timu ya Taifa kama kakosekana yeye hakuna tabu, mbona wakati yeye yupo wenzake walikuwa hawaitwi na ilikuwa kawaida," alisema Mgunda.

Mgunda aliongeza kwa kusema "Kaseja mwenyewe alikosekana kwa takribani miaka sita, lakini leo hii amerejea."

Baada ya kukosekana Manula, benchi la ufundi la timu hiyo limemuita David Kissu anayeichezea Gor Mahia inayoshiriki Ligi Kuu Kenya.

Makipa wengine waliopo katika kikosi hiko ni Kaseja (KMC) na Mnata (Yanga).

Join our Newsletter