Uko hapa: NyumbaniMichezo2019 06 24Article 472503

Sports News of Monday, 24 June 2019

Chanzo: mwananchi.co.tz

VIDEO: Uchambuzi kuelekea mchezo wa Taifa stars na Senegal leo

Dar es Salaam. Wakati Timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ ikijiandaa kukata mzizi wa fitina dhidi ya Senegal Jumapili hii katika mchezo wa kwanza wa Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon), safu ya mabeki ya Senegal inayoongozwa na nyota wa Napoli ya Italia, Kalidou Koulibaly siyo tishio kubwa kulinganisha na ile ya Stars.

Timu hizo zinakata utepe kwenye mchezo wa kundi C ambapo Stars inashiriki kwa mara ya pili fainali hizo baada ya ile ya kwanza mwaka 1980.

Licha ya rekodi ya Senegal na uwepo wa majina ya nyota wanaocheza klabu mbalimbali Ulaya, lakini rekodi ya safu ya ulinzi ya timu hiyo haitofautiani na ile ya Taifa Stars.

Kocha wa Stars, Emmanuel Amunike amewaita mabeki wanane katika kikosi chake wakati kocha wa Senegal, Aliou Cissé aliyewahi kuzichezea PSG na Birmingham City amewajumuisha mabeki saba

Taarifa kamili Usikose nakala ya Mwananchi Leo Jumapili Juni 23, 2019, Tizama pia Video hii--Join our Newsletter