Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 17Article 543166

Habari za michezo of Thursday, 17 June 2021

Chanzo: eatv.tv

VPL michezo mitatu leo, Yanga inashuka dimbani

VPL michezo mitatu leo, Yanga inashuka dimbani VPL michezo mitatu leo, Yanga inashuka dimbani

Ligi Kuu Tanzania bara raundi ya 31, itaendelea tena leo kwa michezo mitatu kuchewa jijini Dar es salaam, Dodoma na huko mkoani shinyanga, mchezo unaosubiliwa kwa hamu ni ule wa Ruvu Shooting dhidi ya Yanga utakao chezwa Saa 1:00 Usiku.

Submitted by Ibra Kasuga on Alhamisi , 17th Jun , 2021 Wachezaji wa Yanga

Mchezo wa mapema unachezwa majira ya Saa 8 mchana. Mwadui FC ambao wameshashuka daraja watakuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar wanao shika nafasi ya 13 kwenye ligi wakiwa na alama 34, mchezo huu unachezwa katika dimba la Mwadui Complex huko mkoani shinyanga.

Saa 10:00 Jioni Dodoma Jiji watakuwa wenyeji wa KMC ya Dar es salaam katika Dimba la Jamuhuri. Timu hizi zinatofautiana alama 2 tu kwenye msimamo, KMC wapo juu wakiwa nafasi ya 6 na alama zao 41 wakati Dodoma wana alama 39 wakiwa nafasi ya 9. Mchezo wa mkondo wa kwanza KMC ilishinda kwa bao 1-0.

Na Mchezo wa Mwisho kesho Ruvu shooting watakuwa wenyeji wa Yanga SC majira ya Saa 1:00 Usiku. Ruvu shooting watakuwa na kibarua cha kufuta uteja mbele ya Yanga, kwani kwenye michezo 8 ya mwisho kukutana wameshinda mara moja tu, na mchezo wa mkondo wa kwanza msimu huu walipoteza kwa kufungwa mabao 2-1.

Ruvu shooting wapo nafasi ya 10 na alama 37, wakati Yanga wana alama 61 wakiwa wanamili nafasi ya pili.