Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 24Article 573907

Soccer News of Wednesday, 24 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Valverde huenda akachukua nafasi ya Ole Man United

Ernesto Valverde Ernesto Valverde

Klabu ya Manchester United wanaripotiwa kufanya mazungumzo ya awali na ikibidi kumchukua aliyekuwa kocha mkuu wa zamani wa Barcelona, Mhispania Ernesto Valverde kuziba pengo lililoachwa na Ole Gunnar Solskjaer.

United wanatafuta meneja mpya baada ya kumtimua alyekuwa meneja wao Ole Gunnar Solskjaer wikiendi iliyopita.

Mashetani hao wekundu walianza vyema msimu huu baada ya kumaliza nafasi ya pili EPL msimu uliopita na kutumia pesa nyingi majira ya joto, lakini hali imekuwa tofauti wiki chache zilizopita wakishuhudia matokeo mabaya katika michezo yao.

Safari ya kumsaka bosi mwingine imehusisha baadhi ya Makocha mahiri kama Zinedine Zidane na Mauricio Pochettino.

Kwa mujibu wa Fabrizio Romano, United imefanya ‘mawasiliano ya moja kwa moja’ na kocha wa zamani wa Barcelona, ​​Valverde.

Valverde amekuwa nje ya kibarua tangu alipoondoka Barcelona mwaka 2020, ingawa kwa makusudi, bosi huyo wa zamani wa Barcelona aliamua kupumzika.

United inaweza kuwa changamoto kwake, lakini kwa mujibu wa ripoti, atachukuliwa tu kama chaguo la muda kuelekea mwisho wa msimu huu.

United wanasemekana kuwa tayari kuajiri bosi wa muda hadi mwisho wa msimu, ingawa haijulikani ikiwa Valverde angefikiria kuchukua jukumu kama hilo kwa muda.