Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 18Article 572371

Soccer News of Thursday, 18 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Van De Beek awatingisha United, kuondoka januari asipojumuishwa kikosini

Kiungo wa Manchester United, Donny Van de Beek Kiungo wa Manchester United, Donny Van de Beek

Kiungo wa Manchester United, Donny Van de Beek, anajiandaa kuondoka kunako klabu hiyo iwapo hatajumuishwa katika michezo ya timu hiyo.

Van de Beek anatarajia kulazimisha uhamisho wake Januari kwani tangu amesajiliwa kutokea Ajax hajakua na uhakika wa namba ndani ya United.

Van de Beek alikuwa akihusishwa na Real Madrid lakini taarifa hiyo imekanushwa na kusemwa tu kuwa kuna timu nyingi zinazohitaji huduma ya kiungo huyo ila bado hakuna mazungumzo yaliyofikiwa.

Donny van de Beek alijiunga na Manchester United, Septemba 2, 2020 akitokea klabu ya Ajax.