Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 29Article 560362

Soccer News of Wednesday, 29 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Vigogo waliobaki Supa Ligi hawana kesi

Klabu ya Barcelona ni miongoni mwa Klabu zilizokuwemo katika Uanzisha wa Supa Ligi Klabu ya Barcelona ni miongoni mwa Klabu zilizokuwemo katika Uanzisha wa Supa Ligi

Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa), limemaliza mpambano wa kisheria dhidi ya klabu za Barcelona, Juventus na Real Madrid uliotokana na timu hizo kujiingiza katika mapendekezo ya kuanzishwa kwa Michuano ya Supa Ligi Ulaya.

Klabu hizo ni miongoni mwa wanachama waanzilishi wa michuano hiyo ambayo baadae ilisambaratika.

Klabu hizo tatu, ambazo zilikataa kuukana mradi huo, zilikuwa zikichunguzwa kwa kutaka kuvuruga mfumo wa kisheria wa Uefa. Uefa inasema shauri hilo lilikuwa halijafunguliwa bado.

"Bodi ya Rufaa ya Uefa leo (jana) inabainisha kuwa kesi hiyo ilikuwa haijafunguliwa,” imesema taarifa hiyo.

Hatua hiyo huenda imekuja baada ya mahakama jijini Madrid kubainisha kuwa Uefa hawakutakiwa kuziadhibu klabu hizo tatu zilizobaki katika mradi huo.

Inaelezwa kuwa Barca, Real na Juventus zimeachiwa huru baada ya mahakama jijini Madrid kuzuia kuchukuliwa kwa hatua yoyote dhidi ya Supa Ligi kwa sababu hiyo inawakilisha biashara huru Ulaya.