Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 22Article 573598

Soccer News of Monday, 22 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Vilabu Vitatu vya EPL Vinataka Saini ya Ramsey

Ramsey asakwa EPL Ramsey asakwa EPL

Mchezaji wa Juventus Aaron Ramsey anajiandaa kumaliza mkataba wake na klabu ya Juventus na kurejea katika Premier League na amekuwa na wakati mgumu huko Turin tangu ajiunge na klabu hiyo ya Serie A mwaka 2019 kama mchezaji huru.

Na vilabu vilivyoonyesha kumtaka kiungo huyo ni Arsenal, Newcastle na Tottenham na The Gunners huenda wakashinda katika kinyang’anyiro hicho kwa mchezaji wao zamani.

Mikel Arteta anajaribu kuijenga timu ya vijana yenye nguvu lakini pia anahitaji vichwa venye uzoefu kama Ramsey ambaye anaijua vizuri Arsenal.

Spurs ambao ni mahasimu wakubwa wa Arsenal pia wameonyesha nia ya kuipata saini ya kiungo huyo lakini je mashabiki wa Spurs watampokea? Kwani Ramsey aliwahi kukataa kujiunga na Tottenham alipoulizwa na mwaka 2018 kama angeweza kuhamia Spurs alijibu hapana.

Matajari wapya wa EPL Newcastle wanataka majina makubwa sasa kwenye timu yao kwani wanao uwezo wa kumudu mishahara mikubwa, hii inamaaanisha Ramsey anaweza kwenda Newcastle.