Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 03Article 540790

Habari za michezo of Thursday, 3 June 2021

Chanzo: ippmedia.com

Wabongo wamponza Samatta kurejea Villa

Wabongo wamponza Samatta kurejea Villa Wabongo wamponza Samatta kurejea Villa

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Samatta ambaye mkataba wake wa mwaka mmoja wa mkopo na Fenerbahce ya Uturuki unamalizika, ameonyesha wasiwasi kama anaweza kudumu sana Aston Villa kutokana na maneno ambayo Watanzania waliyaandika wakati anaondoka kuelekea Uturuki.

"Watanzania baada ya kuondoka Aston Villa waliongea maneno makali sana, kwa hiyo sijui kama nikirudi nitakaribishwa au nitafukuzwa. Nadhani nitarudi lakini sijui kama nitakaa kwa sababu Watanzania bwana, wengi waliongea maneno makali sana, sasa huwezi jua kama watakuwa wamenikasirikia," alisema Samatta.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), aliondoka Aston Villa mwanzo mwa msimu huu baada ya kuichezea timu hiyo ya Ligi Kuu England kwa miezi sita tu, huku akiwa amesaini mkataba wa miaka minne na nusu.

Nyota huyo wa zamani wa African Lyon, alijiunga na Aston Villa, Januari mwaka 2020 akitokea KRC Genk ya Ubelgiji.

Baada ya kujiunga, Watanzania wengi waliingia katika akaunti za mitandao rasmi ya kijamii ya Aston Villa na kuandika ujumbe wa kuishabikia timu hiyo, lakini baadaye waligeuka na kuwa mwiba kufuatia kutangazwa nyota huyo anatolewa mkopo.

Baadhi ya maneno ya mashabiki hao yalilenga kuonekana mchezaji huyo ananyimwa ushirikiano na wachezaji wenzake kama vile kupewa pasi akiwa kwenye nafasi ya kufunga, hivyo kuwanyooshea vidole baadhi ya wachezaji wa timu hiyo.

Hali hiyo ilileta mkanganyiko hadi Samatta mwenyewe alilazimika kuandika ujumbe wa kuwatuliza mashabiki wake kwa kuwasihi waache tabia ya kuwashukutumu wachezaji wenzake, kitu ambacho pia kilipingwa na mashabiki hao, wakimtaka acheze soka, kazi ya mitandao ya kijamii awaachie wao.

Hata alipoondoka kwenda Fenerbahce, baadhi ya Watanzania waliandika maneno makali, ikiwamo wengine kujiondoa kwenye ukurasa wa mtandao wa klabu hiyo.

Join our Newsletter