Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 14Article 551542

Soccer News of Saturday, 14 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Wachezaji wa Kigeni sasa ni 12

Ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF) limepitisha kanuni mpya leo,kuhusiana na idadi ya usajili kwa wachezaji wa kigeni na wale ambao wanatakiwa kuanza katika mchezo mmoja.

Katika mabadiliko hayo, timu zinaruhusiwa kusajili wachezaji 12 wa kigeni na 8 tu wanaruhusiwa kucheza kwenye mechi moja.

Mabadiliko hayo yamepokelewa kwa hisia tofauti na mashabiki wa soka hapa nchini wakidai itawapa faida zaidi wagteni huku wazawa wakikosa nafasi na zaidi wamekwennda mbali na kudai kuwa kanuni hiyo inadhoofisha timu yetu ya taifa.

Kabla ya mabadililko hayo ya kanuni yaliyotokea ama kufanyika hii leo, timu zilikua zinaruhusiwa kusajili wachezaji kumi (10) wa kigeni na saba wanaruhusiwa kuanza katika mvhezo mmoja.