Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 19Article 572635

Soccer News of Friday, 19 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Wachezaji wa Tanzania wang'ara COSAFA

Erick Manyama Erick Manyama

Mtanzania Erick Manyama amechaguliwa Mchezaji Bora wa Mechi ya Kundi B michuano ya COSAFA Soka la Ufukweni akiiwezesha timu yake ya taifa kushinda 2-1 dhidi ya Comoro Alhamisi Jijini Durban, Afrika Kusini.

Tanzania imefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya michuano hiyo baada ya kufanya vizuri katika mechi zake mbili za Alhamisi ufukwe wa South Beach Arena Jijini Durban, Afrika Kusini.

Baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Comoro, Tanzania ilifungwa kwa penalti 4-3 na Msumbiji kufuatia sare ya 4-4 South Beach Arena.

Sasa Tanzania itamenyana na Angola katika mechi ya Nusu Fainali Ijumaa hapo hapo South Beach Arena, wakati Msumbiji itamenyana na wenyeji, Afrika Kusini katika Nusu Fainali nyingine.