Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 22Article 552919

Soccer News of Sunday, 22 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Wadau walalamikia ratiba Ligi kuu Bara

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Wadau mbali mbali wa masuala ya Soka nchini, wamelalamikia namna bodi ya Ligi inavyopanga ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara, huku ikionekana kuwa rafiki kwa Klabu kongwe nchini za Simba na Yanga.

Wadau hao wa Soka wametoa rai hiyo kuhusiana na namna mechi za ligi kuu Tanzania bara zinavyochezwa na hasa katika suala zima la muda.

wadau hao wametoa malalamiko hayo kwa lengo la kutaka kuwepo na ushindani sawa katika ligi huku wakitoa mifano kuwa kuna timu nyingi zinacheza baadhi ya michezo yao saa nane mchana lakini ni tofauti pindi linapokuja suala la Simba na Yanga.

Muda wanaocheza Simba na Yanga ni muda rafiki sana lakini hatujawahi kuwaona wakicheza mechi zao mchana wa jua kali kama kwenye baadhi ya mechi za vilabu vingine.

"Hatusemi kwamba sio bora, lakini chochote kinachofanywa kwa wenzao na wao wafanyiwe kusiwe na mazingira tofauti kwa kuwa wote ni washindani katika ligi angalau itatupa heshima kwa wenzetu wanaofatilia ligi yetu" amesema mmoja wa wadau hao.

Kuna taarifa kuwa Klabu za Simba na Yanga hazijawahi kupangiwa mechi muda wenye jua kali tofauti na timu nyingine ambazo mara kwa mara zinacheza mpaka saa nane mchana.

Hivyo wameitaka TFF kuhakikisha wanalishughulikia suala hilo kabla msimu mpya wa ligi haujaanza ili kupunguza lawama zisizo na msingi.