Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 21Article 573217

Soccer News of Sunday, 21 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Walcot ana imani na maamuzi ya Ramsey

Walcot akiwa na Ramsey wakiwa Arsenal Walcot akiwa na Ramsey wakiwa Arsenal

Winga wa zamani wa Arsenal Theo Walcott ambaye kwa sasa anawika na kikosi cha Southampton amempigia chapuo mchezaji mwenzake wa zamani katika kikosi cha Gunners Aaron Ramsey kurejea Epl

Kiungo huyo wa Wales ,Ramsey,30, miaka miwili iliyopita alitua katika kikosi cha Juventus lakini kwa sasa mambo yanamuendea kombo baada ya kukumbwa na balaa la majeraha sambamba na kutopata nafasi ya kucheza mara kwa mara hasa msimu huu

Theo amesema kuwa anamuelewa sana Ramsey hasa kile anachokifikiria juu ya kurejea katika ligi kuu soka nchini England na haoni sehemu nyingine zaidi ya kurejéa Arsenal sehemu ambayo amekaa zaidi ya misimu 10 tangu aliposajiliwa mwaka 2008 akitokea Cardiff city na mzee Arsene Wenger

Walcott ameyasema hayo kwenye kipindi hiki ambacho kiungo huyo mwenye michezo 77 katika kikosi cha Wales kuhusishwa kuwa mbioni kujiunga na Newcastle united.