Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 07 20Article 547723

Michezo Mingine of Tuesday, 20 July 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Waliooa v Wasiooa Kivumbi Kama Kawa

Waliooa v Wasiooa Kivumbi Kama Kawa Waliooa v Wasiooa Kivumbi Kama Kawa

KIVUMBI kama kawa wanasema kinazidi kutimka ambapo kwa sasa kila mmoja anahesabu siku kabla ya ule mchezo wa kukata na kisu kuchezwa kati ya Waliooa v Wasiooa unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Sinza, Julai 30.

Ni timu zenye ubishi kutoka Global Group zimeingia kwenye kambi matata Bongo na lengo ni kuongeza nguvu kwenye kusaka ushindi kuelekea mchezo huo ambao unasubiriwa kinomanoma na wadau.

Waliooa ni noma, waliwachapa kwa mbinu mabao 2-1 Wasiooa hivyo mchezo ujao utakuwa kwenye mwendo wa tofauti kwa kila timu kuja kivingine kabisa.

Wasiooa wanatambia uwepo wa sapoti kutoka kwa Smart Gin na Creative Bee ambao watatoa jezi na zawadi kedekede pia Peak Time Media hawapo nyuma, Tukuyu Spring Water, Global TV na +255 Global Radio wameweka mkono wao wa nguvu huku kwa wale Waliooa wapo na Saleh Jembe Blog.

Hussein Msoleka, Ofisa Habari wa Wasiooa, alisema kikosi kazi kipo imara na watawashtua wale wapinzani wao kwa kupiga pira la maana ambalo litawashushia mabao ya kutosha zaidi ya mvua.

Kwa Waliooa ni Wilbert Molandi mchezaji ghali chaguo namba moja wa kikosi hicho, alisema kuwa hawatishwi na tambo za vijana wadogo ambao bado hawajajua mbinu za mpira zinavyokuwa ndani ya uwanja.

#EXCLUSIVE MKE wa CAPTAIN KOMBA Amuomba WAZIRI MKUU – “USINICHOKE, NISAIDIE Kupata FIDIA ZANGU”

Share this:TweetWhatsApp Related