Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 22Article 559075

Sports Features of Wednesday, 22 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Wanamichezo walioingiza mkwanja mrefu 2021

Miongoni mwa wanamichezo walioingiza fedha nyingi kwa mwaka 2021 Miongoni mwa wanamichezo walioingiza fedha nyingi kwa mwaka 2021

Wanamichezo maarufu Duniani hawaingizi fedha kutokana na michezo wanayoshiriki tu, bali pia kutokana na Ufadhili wa Makampuni mbali mbali ya udhamini na Matangazo.

Wataalamu wa masuala ya Michezo ulimwenguni wanaonesha namna ambavyo wanamichezo wanaweza kutumia umaarufu wao kuweza kuingiza kiasi kikubwa cha fedha. Ifuatayo ni orodha ya wanamichezo 10, walioongoza kwa kuingiza fedha nyingi kwa mwaka 2021, na hii ni kwa mujibu wa jarida maarufu la Forbes.

10. Kevin Durant ( Dolla za Kimarekani Milioni 75)

Huyu ni nyota wa mpira wa kikapu wa timu ya Brooklyn Nets inayoshirki NBA nchini Marekani, ameingiza kiasi cha Dola milioni 31 uwanjani na dola milioni 44 kutoka katika vyanzo vingine.

Nyota huyo amewekeza katika makampuni zaidi ya 40 yakiwemo ya kutoa huduma za vyakula na kampuni za huduma za kifedha.

9. Tom Brady (Dola za Kimarekani Milioni 76)

Tom Brady amebeba ubingwa zaidi ya mchezaji yeyote katika historia ya NFL. Bingwa huyo mara saba wa Supe Bowl ameingiza kiasi cha Dola za kimarekani milioni 45 kutokana na mchezo huo huku kiasi cha dola milioni 31 nje ya mchezo huo ndani ya miezi 12 iliyopita.

Brady anatangaza na Makampuni makubwa ulimwenguni kama Under Armour, Tag Heuer na Aston Martin.Pia anamiliki kampuni yake ya uzalishaji wa Vipindi aliyoizindua mwaka 2020.

8. Sir Lewis Hamilton (ameingiza Dola za Kimarekani Milioni 82)

Dereva wa mbio za magari yaendayo kasi maarufu kama Langa langa. Ameingiza kiasi cha Dola za kimarekani milioni 70, kutokana na Mashindano na ameongeza Mkataba wa mwaka mmoja na Kampuni ya Marcedes inayoshiriki michuano ya Formula 1.

Hamilton ameingiza kiasi cha dola milioni 12, kutokana na mikataba ya Matangazo ya bidhaa za Tommy Hilfiger.

7. Roger Federer (ameingiza Dola za Kimarekani Milioni 90)

Nyota wa Tennis kutoka nchini Uswiss, amekosa michuano ya US Open kutokana na majeraha ya kifundo cha Mguu, lakini ameingiza kiasi kikubwa cha fedha kutokana na mikataba yake ya matangazo na Makampuni makubwa kama Rolex, Marcedes- Benz , Vile vile Federer ana mkataba wa miaka 10 na Kampuni ya nguo kutoka nchini Japan wenye thamani ya Dola za Kimarekani Milioni 300.

6.Neymar (ameingiza Dola za Kimarekani Milioni 95 )

Nyota wa Soka kutoka Brazil anayekipiga kunako klabu ya PSG ya nchini Ufaransa. Ameingiza kiasi cha Dola za kimarekani milioni 76 kutokana na Mkataba wake ndani ya PSG, Mwezi Mei mwaka huu, amesaini Mkataba utakaomfanya adumu ndani ya klabu hiyo mpaka mwaka 2025.

Neymar ameingiza kiasi cha Dola za kimarekani milioni 19 kutokana na mikataa ya matangazo na kampuni za Puma na Epic Games.

Neymar ndio mchezaji anaeshikilia rekodi ya kununuliwa kwa pesa ndefu (Dola milioni 263) alipotoka Barcelona kwenda PSG.

5. LeBron James ( ameingiza Dola za Kimarekani Milioni 96.5)

Nyota mwingine wa Mpira wa Kikapu anayekipiga kunako timu ya L.A Lakers. Mkataba wake na timu hiyo unamuacha akiingiza benki kiasi cha Dola za kimarekani milioni 31.5 lakini James , ameigiza hadithi ya nguli wa mchezo huo, Michael Jordan, jambo ambalo limemshuhudia Le bron akiingiza kiashi cha Dola milioni 65.

LeBron pia ana mikataba tofauti tofauti ya matangazo na anaendesha biashara nyingi zikiwemo za uzalishaji wa vipindi na matangazo, Vyombo vya Habari, migahawa ya pizza na nyingine nyingi ambavyo ni moja ya vyanzo vyake vya mapato.

4. Dak Prescott (ameingiza Dola za Kimarekani milioni 107.5 )

Mwaka 2021, Dak Prescott alirefusha mkataba wake na kuongeza miaka minne zaidi na klabu ya Dallas Cowboys wenye thamani ya Dola za kimarekani 160. Ili kurahisisha makubaliano na mchezaji huyo aliongezwa kiasi cha ziada cha dola milioni 66.

Kwa mwaka huo tu ulimfanya mwanamichezo huyo kupokea kiasi cha dola milioni 97 na dola milioni 10 kutoka katika mikataba ya matangazo na makampuni tofauti tofauti.

Mei mwaka huu, alitangaza uwekezaji wake katika migahawa ya WalK-On's restaurant iliyopo Texas.

3. Cristiano Ronaldo (ameingiza Dola za Kimarekani milioni 120 )

Mkongwe huyo anaekipiga katika Klabu ya Man United kwa sasa ameingiza kiasi cha Dola za kimarekani milioni 70 kutokana na mishahara na nyongeza ya malipo mbali mbali.

Nje ya Soka Ronaldo ameingiza kiasi cha dola milioni 50, kutokana na mikataba yake ya matangazo na Nike na kampuni zake binafsi za mavazi CR7 clothes , Hoteli na sehemu za kufanyia mazoezi.

2. Lionel Messi (ameingiza Dola za Kimarekani Milioni 130 )

Nyota mwingine wa mchezo wa mpira wa miguu na mshindi wa Tuzo za mchezaji bora wa Ulaya mara sita ambae amekunja kiasi cha Dola za Kimarekani milioni 97 kutokana na Soka kwa mwaka 2021.

Messi amejiunga na PSG dirisha la usajili lililopita na mshahara wake kwa mwaka unakadiriwa kuwa ni Dola za kimarekani milioni 75, na hiyo haijumuishi nyongeza wala mauzo ya vifaa mbali mbali vya mivchezo kama jezi na vifaa vingine.

Messi ameingiza kiasi cha dola milioni 33, nje ya uwanja na ikumbukwe messi ana mkataba wa Maisha na Kampuni ya Adidas.

1. Conor McGregor (ameingiza Dola za Kimarekani milioni 188) Nyota wa masumbwi, Mixed Martial Arts, Conor McGregor, amepigana katika pambano moja tu mwaka huu na amepoteza, lakini hilo halikuzuia kuingiza kiasi cha Dola milioni 22 katika akaunti yake.

Nyota huyo ameingiza kiasi cha Dola Milioni 158 nje ya ulingo na hiyo ni kutokana na kuuza hisa zake katika Kampuni ya Whiskey, Proper No. Twelve mwezi April.