Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 15Article 586117

Soccer News of Saturday, 15 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Wapewe tu Kombe lao! Maana wanaupiga mwingi

Goli pekee la City, limewekwa wavuni na Kevin De Bruyne Goli pekee la City, limewekwa wavuni na Kevin De Bruyne

Ebwana! Manchester City hawakamatiki. Ndio ukweli baada ya hii leo Januari 15, kuwachapa Chelsea bao 1-0 katika Dimba la Etihad.

Goli pekee la ushindi limefungwa na Kiungo wa Kibelgiji Kevin De Bruyne, dakika ya 70 ya mchezo akipiga shuti kali lililomuacha golikipa Kepa Arrizabalaga akiwa hana la kufanya.

Katika mchezo wa leo City walifanya kila Jambo kwa usahihi, kitu kilichowapa wakati mgumu Chelsea muda wote wa mchezo.

Mshambuliaji wa Chelsea Rumelu Lukaku almanusura awasawazishie Chelsea kama si uhodari wa golikipa wa City Ederson, alieokoa mpira uliokoa unakwenda nyavuni.

Kwa ushindi huo wa leo, Man City inazidi kujitengenezea mazingira ya kutetea taji la EPL baada ya kuongeza tofauti ya alama 13 kati yake na mtu wa pili ambae ni Chelsea.

Man City kwa sasa amejikusanyia alama 56 baada ya kushuka dimbani mara 22 akifuatiwa na Chelsea mwenye alama 43 huku nae akiwa ameshacheza michezo 22.