Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 29Article 554248

Soccer News of Sunday, 29 August 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

"Watanzania hawanidai" - Kaseja

Juma Kaseja, Golikipa wa zamani wa Taifa Stars Juma Kaseja, Golikipa wa zamani wa Taifa Stars

Kipa mkongwe, Juma Kaseja amesema kwa kipindi ambacho amelitumikia soka la Tanzania anaamini kuwa hana deni kutokana na mchango wake mkubwa aliouonyesha.

Kaseja ambaye kwa sasa anakipiga KMC, amesema anachohitaji kwa sasa kwa Watanzania ni heshima kwani amefanya makubwa na kuonyesha thamani yake katika klabu mbalimbali ambazo amezitumikia pamoja na timu ya Taifa.

“Naamini nimefanya mambo mengi kwenye mpira wa Tanzania jambo ambalo kila uchao linanipa faraja nikiona michezo nchini inapiga hatua, hivyo kwa sasa ninachohitaji ni heshima tu maana Watanzania hawanidai,” amesema Kaeja.

Kuhusu malengo ya msimu mpya, Kaseja amesema timu yao inajiandaa kufanya vizuri zaidi tofauti na msimu uliopita.

“Msimu uliomalizika tulimaliza nafasi ya tano, haikuwa nafasi nzuri sana kwa sababu tulihitaji kufanya vizuri zaidi ya hapo, ila naamini msimu huu tutasogea katika nafasi tatu za juu,”

Kuhusu ushindani, Kaseja alisema utakuwa mkubwa sana kwa sababu kila timu imejiandaa vizuri lakini hata suala la uwekezaji kwa klabu ni mkubwa.

“Klabu kwa sasa zina fedha ya kutosha katika kujiendesha kutokana na udhamini ambao TFF wameingia hivyo ushindani utakuwa mkubwa maana timu nyingi zitakuwa zinajiweza kwenye kulipa mishahara wachezaji wake.”