Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 19Article 558388

Habari za michezo of Sunday, 19 September 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Wawili wapya waanza Simba dhidi ya TP Mazembe

Wawili wapya waanza Simba dhidi ya TP Mazembe Wawili wapya waanza Simba dhidi ya TP Mazembe

Muda mchache kabla ya pambano la kimataifa la kirafiki kati ya Simba dhidi ya TP Mazembe kuanza, vikosi vya timu zote mbili vilitambulishwa.

Kikosi cha Simba kilianza na wachezaji wawili wapya ambao ni, kiungo wa Mali Sadio Kanoute na straika Kibu Denis.

Wachezaji wengine wote waliobaki walikuwepo katika kikosi cha Simba msimu uliopita na walikuwa wakianza mara kwa mara.

Kipa Aishi Manula alianza huku mabeki wake wanne walikuwepo, Shomary Kapombe, Mohammed Hussein, Pascal Wawa na Joash Onyango.

Katika eneo la kiungo walianza watatu ambao walikuwepo, Kanoute, Bwalya ambao kiasili ni wakabaji zaidi huku juu yao alikuwepo, Rally Bwalya.

Katika eneo la washambuliaji walikuwepo watatu, Bernard Morrison, Chriss Mugalu na Kibu.

Aishi Manula Shomari Kapombe Mohammed Hussein Joash Onyango Pascal Wawa Taddeo Lwanga Sadio Kanoute Chriss Mugalu Larry Bwalya Kibu Denis Bernard Morrison