Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 20Article 552649

Soccer News of Friday, 20 August 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Wazir Junior avunja mkataba na Yanga

Mshambuliaji wa Yanga, Waziri Junior ambae anasadikiwa kuvunja Mkataba Mshambuliaji wa Yanga, Waziri Junior ambae anasadikiwa kuvunja Mkataba

Aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga Wazir Junior amewaaga mashabiki wa timu hiyo baada ya kuthibitisha kuachana nao kwa msimu ujao.

Kupitia mtandao wake wa Instagram Junior ameandika

"Nichukue fursa hii kuwashukuru sana wana Yanga kuanzia makocha, wachezaji, viongozi na mashabiki kwa kuniamini na kuwa mmoja wao, haikuwa safari rahisi licha ya kuwa fupi mno,"

"Nilifika Yanga SC nikiwa na malengo makubwa lakini haikwenda kama nilivyotarajia labda kwa sababu zangu binafsi au vinginevyo, ni kawaida yetu sisi wanasoka kukutana na changamoto kama hizi nimechukua maumuzi mgumu sana kwangu lakini yote ni kwa maslahi mapana ya ufanisi wangu," amesema.

Nyota huyo amesema kuwa hakuweza kufikia malengo aliyotoa kwa mashabiki lakini amewatoa shaka kwa sababu haikuwa dhamira yake kuwaangusha kwani anajivunia kuvaa nembo ya klabu kubwa hapa nchini hivyo kuamua kuhamishia jitihada zake sehemu nyingine.

"Yamkini sikufikia malengo ya klabu na kutokuwapa mashabiki ile furaha waliyotarajia kutoka kwangu lakini niwatoe shaka kuwa haikuwa dhamira yangu kuwaangusha," alisema.

"Niwatakie kila la kheri kwenye safari yenu kuelekea msimu ujao. Tuendelee kuombeana labda ipo siku tutakuwa pamoja tena kama sio, basi nitaendelea kuuenzi upendo na imani mliyoijenga kwangu," amesema.

Taarifa za uhakika zinadai kuwa Mkataba wa Waziri na Yanga bado haujamalizika ila tu nyota huyo ameamua kuvunja ili atafute timu atakayopata nafasi ya kucheza mara kwa mara.