Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 18Article 572593

Soccer News of Thursday, 18 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Xavi majaribuni wikendi hii

Kocha mpya wa Barca, Xavi Hernandez Kocha mpya wa Barca, Xavi Hernandez

Mashabiki wa sehemu mbalimbali duniani kwa sasa wanasubiri kumuona Xavi akiwa kwenye benchi la Barcelona na kubeba mzigo uliowashinda wenzia kwenye viunga vya Camp Nou.

Baada ya kufanya vizuri nchini Qatar na style ya "tiktak" ambayo iliasisiwa na Johan Cryuf na kutumiwa vizuri kabisa na kocha wa kihispania Pep Gurdiola sasa mashabiki wanahamu ya kuona Xavi akiirudisha tena kwenye viunga vya Camp Nou.

Barcelona wikiendi hii wanawakaribisha klabu ya Espanyol kwenye dimba la Camp Nou huku baadhi ya wachezaji nao wakirejea kutoka kwenye michezo ya kimataifa na wale majeruhi Pedri na Dembélé wakitarajiwa kurudi kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Benfica.

Xavi tokea achukue mikoba ya kuinoa klabu hiyo amefanya mabadiliko makubwa huku akitumbua majipu ambayo alihisi ni kikwazo kwa mafanikio ya Barcelona.