Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 20Article 573073

Soccer News of Saturday, 20 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Yanga Chupu Chupu kwa Namungo, yalazimisha sare

Mfungaji wa Goli la kusawazisha kwa Yanga Mfungaji wa Goli la kusawazisha kwa Yanga

Vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Primia Ligi), Yanga SC wamepunguzwa kasi hii leo baada ya kutoa sare ya 1-1 na wenyeji, Namungo FC katika Uwanja wa Ilulu mjini Lindi.

Namungo FC walitangulia kwa bao safi na la kiufundi la mshambuliaji Mzambia, Obrey Chirwa akiifunga timu yake ya zamani dakika ya 53, kabla ya kiungo Saido Ntibanzokiza kumfunga Mrundi mwenzake, kipa Jonathan Nahimana kwa penalti dakika ya 82.

Kikosi cha Namungo kilishuhudia wakimaliza pungufu baada ya nyota wake akilimwa kadi nyekundu.

Yanga inafikisha pointi 16 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi mbili zaidi ya mabingwa watetezi, Simba SC baada ya timu zote kucheza mechi sita.