Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 07Article 541354

Habari za michezo of Monday, 7 June 2021

Chanzo: ippmedia.com

Yanga: Hatutaki Simba itubebe michuano CAF

Yanga: Hatutaki Simba itubebe michuano CAF Yanga: Hatutaki Simba itubebe michuano CAF

-zilizotengenezwa na watani wao hao wa jadi.

Kufanya vizuri kwa Simba kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kumeiwezesha Tanzania kushika nafasi ya 12 katika viwango vya CAF, hivyo kuwa kati nchi 12 zitakazoingiza timu nne kwenye michuano ya shirikisho hilo; Ligi ya Mabingwa mbili na idadi kama hiyo Kombe la Shirikisho Afrika.

Hiyo ni baada ya kufikisha pointi 27.5 ikiiacha mbaliĀ  Senegal inayoshika nafasi ya 13 kwa pointi 15, hivyo sasa timu mbili zitaongezeka msimu ujao kutoka moja iliyokuwa ikishiriki Ligi ya Mabingwa na moja Kombe la Shirikisho.

Katika msimu wa 2017/18, wakati Yanga ilipokuwa ikiiwakilisha Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa, iliambulia kuvuna pointi moja tu, lakini msimu wa 2019/20, Simba ikaiwezesha nchi kupata pointi tisa kisha msimu huu ikiongeza pointi 15 baada ya kufika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa, wakati Namungo iliyotinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho msimu huu ikiiongezea Tanzania pointi 2.5.

Na kwa mujibu wa kanuni za Shirikisho la Soka nchini (TFF), bingwa wa Ligi Kuu Bara, huiwakilisha nchi kwenye Ligi ya Mabingwa wakati mshindi wa FA Cup, hubeba jukumu la kuipeperusha bendera ya nchi kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.

Lakini kutokana na kuongezeka kwa timu na kuwa nne, mshindi wa pili wa Ligi Kuu ataongozana na bingwa kuiwakilisha nchi kwenye Ligi ya Mabingwa huku timu itakayoshika nafasi ya tatu ikiambatana na mshindi wa FA Cup kwenda kucheza Kombe la Shirikisho Afrika.

Tayari Simba ipo katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kutokana na kuwa na pointi 67, sita mbele ya Yanga iliyopo nafasi ya pili huku ikiwa mbele michezo miwili na Azam ikishika nafasi ya tatu na alama zake 60 baada ya kushuka dimbani mara 30.

Hivyo, kutokana nafasi hizo ambazo Simba imezitengeneza, mashabiki na viongozi wa klabu hiyo wanaamini timu mbili zitakazoshiriki michuano hiyo kama si kwa njia ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ama Kombe la FA, zitakuwa zimekwenda kwa mgongo wao.

Lakini Mkurugenzi wa uwekezaji wa Gsm, ambao ni wadhamini wa Klabu ya Yanga, Injinia Hersi said, amesema wana uhakika wa kutwaa Kombe la FA na kwenda kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika pasipo kutegemea nafasi hizo zilizotengenezwa na Simba.

"Hatuiandai Yanga kwa kuiangalii Simba, hatutegemei pia mtu kucheza mashindano ya CAF, haijalishi wametengeneza nafasi ngapi, sisi tutaifunga Biashara na kucheza fainali.

"Mshindi kati ya Simba na Azam tutamfunga fainali na kutwaa Kombe la FA na kwenda kucheza Kombe la Shirikisho Afrika bila kumtegemea mtu yeyote," alisema Hersi.

Aidha, alisema pia anajivunia mambo makubwa ambayo Yanga imefanikiwa ikiwamo kutwaa Kombe la Mapinduzi mbele ya mahasimu wao, Simba.

Yanga itacheza nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Biashara United wakati Simba ikicheza dhidi ya Azam FC na washindi wa mechi hizo mbili watakutana fainali.

Join our Newsletter