Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 24Article 544051

Habari za michezo of Thursday, 24 June 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Yanga Manzese wataka kamati ya ufundi kuokoa MaPro wao

Yanga Manzese wataka kamati ya ufundi kuokoa MaPro wao Yanga Manzese wataka kamati ya ufundi kuokoa MaPro wao

UNAIJUA kamati ya ufundi wewe? Sasa wanachama Wa Yanga tawi la Beston Manzese wameutaka uongozi wa klabu hiyo kuchangamka ili kuwanusuru wachezaji wao hasa wa kimataifa wanaosajiliwa na klabu hiyo na ghafla na wanakuwa magalasa.

Mmoja ya wajumbe wa tawi hilo, Ibrahim Ngatunga alisema haiwezekani wachezaji wa kimataifa wanaosajiliwa na klabu hiyo kila wakifika hapa nchini viwango vyao vinapotea ghafla hivyo, lazima jambo lifanyike ili kuwalinda.

“Huwa tunajiuliza inakuaje mchezaji anakuwa mfungaji bora huko nchini kwao au ana kiwango kikubwa na tunamsajili lakini akifika hapa hakuna anachofanya.

“Jambo hilo huwa linatuumiza sana hivyo ushauri wetu kwa uongozi ni wakishasajili hao wachezaji watumie kamati ya ufundi, sio ya uwanjani ila’ yale mambo yetu yale’ ili kuwakinga wachezaji wetu maana haiwezekani lazima kuna namna,” alisema Ngatunga.

Mjumbe mwingine wa tawi hilo, Ramadhan Athuman alisema timu hiyo inahitaji kuongeza wachezaji katika nafasi sita msimu ujao ambao ni kipa, beki zote za pembeni, kiungo na washambuliaji wawili.

Pia Athuman alisema Julai 3 hawataingiza timu uwanjani kuikabili Simba hadi pale watakapopata sababu muhimu ya kwa nini mechi ya Mei 7 ilihairishwa.

Naye mwanachama mwingine wa tawi hilo Honorascus Justinian alizungumzia kuhusu kipa wa timu hiyo Metacha Mnata ambaye amesimamishwa kuwa ni wakati wake kuondoka ndani ya klabu hiyo.

“Metacha ni kama ana kitu moyoni, ni kipa mzuri lakini viti anavyovionyesha ni kama Yanga sio sehemu sahihi kwake tena kwa sasa yaani anafanya vitu ili afukuzwe,” alisema Honorascus.

SAFU YA UONGOZI

Tawi hilo ambalo ni la muda mrefu limepangwa kuzinduliwa upya Julai mwaka huu na lina wanachama 65.

Tawi la Beston Manzese linaongozwa na viongozi wa muda ambao ni mwenyekiti, Ramadhan Unga, Katibu ni Miki Mchiro na mtunza hazina ni Issa Stopper.