Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 19Article 572845

Soccer News of Friday, 19 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Yanga SC yatua Lindi, Kuwavaa Namungo FC

Kikosi cha Yanga kipo Lindi kuvaana na wenyeji Namungo FC Kikosi cha Yanga kipo Lindi kuvaana na wenyeji Namungo FC

Klabu ya Yanga SC imewasili mkoani Lindi kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo FC ambao utapigwa Jumamosi, Novemba 20 katika uwanja wa Ilulu.

Yanga SC wamepata maandalizi ya kutosha kuelekea mchezo huo ambapo wiki iliyopita walikuwa visiwani Zanzibar ambako walialikwa kwenye maadhimisho ya Mwaka mmoja Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Rais Dk Hussein Ali Mwinyi.

Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi alieleza kufurahishwa na kambi ya siku tano waliyoweka Zanzibar ambapo waliweza kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Mlandege na KMKM wakiibuka na ushindi wa 1-0 na 2-1.

Nabi amepania kuvunja rekodi ya Yanga SC dhidi ya Namungo kwani michezo minne iliyopita baina ya timu hizo haikutoa mshindi.

Namungo ni moja ya timu zilizofanya usajili mzuri ikiwa na baadhi ya wachezaji ambao wamewahi kutamba Yanga kama Obrey Chirwa, David Molinga, Abdulaziz Makame na Mohammed Issa ‘Banka’.