Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 17Article 558088

Habari za michezo of Friday, 17 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Yanga: Tumejiandaa Kisaikolojia

Haji Manara Haji Manara

Msemaji wa Klabu ya Yanga, Haji Manara amesema maadalizi ya mchezo wao wa marejeano, hatua za awali dhidi ya Rivers United yamekamilika na wamejiandaa kwenda kupambana na kupindua matokeo ili waweze kusonga mbele katika hatua ya pili ya michuano hiyo.

Manara amesema hayo leo, Ijumaa, Septemba 17, 2021 wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar kuelekea mechi hayo ambapo Yanga wakiwa nyumbani, Jumapili iliyopita walipoteza mchezo wa kwanza kwa kukubali kichapo cha bao 1-0.

“Tunaenda kucheza mechi ambayo kwa vyovyote vile itakuwa ngumu, mechi za ugenini kwenye ligi ya mabingwa siku zote huwaga ni ngumu na hilo jambo tunalitarajia.

“Tunajua mechi za ugenini zina visa na mikasa mingi, kisaikolojia tumejipanga na tumejiandaa na hilo na ndiyo maana tulituma watu imara wakufanya maandalizi yote kabla ya timu kufika.

Yanga wanatarajia kusafiri leo kwa ndege ya kukodi kwenda Nigeria ambapo mchezo wao utapigwa Jumapili, Septemba 19, 2021.

Akizungumzia Yanga kuingia makubaliano na Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), Manara amesema; "Leo nimesikia kuna wenzetu nao wamekwenda ATCL sisi tuna makubaliano nao muda mrefu sana hatujaanza leo" - Haji Manara Msemaji wa Yanga,” amesma Manara.