Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 22Article 573529

Habari za michezo of Monday, 22 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Yanga Waangukia Pua Kesi ya Morrison, CAS Yatoa Maamuzi

Morrison Morrison

Mchezaji wa Simba, Bernard Morrison ameshinda kesi ilipelekwa na klabu ya Yanga katika mahakama ya usuluhishi wa Michezo (CAS).

Yanga walipeleka kesi hiyo CAS baada ya kutoridhishwa na maamuzi ya kamati ya haki na maadili na hadhi ya Wachezaji ambayo ilitoa hukumu kuwa mkataba wa Yanga na Morrison ulikuwa na mapungufu hivyo ikaruhusu usajili kwenda Simba.

Kwa upande wao Yanga wamekuwa wakisisitiza kuwa Morrison ni mchezaji wao halali. Morrison alisajiliwa Yanga katika dirisha dogo 2019/2020, ambayo aliitumikia kwa miezi kadhaa kabla ya kutimkia Simba.